Habari Mseto

Elimu: Jumwa asaidia wasichana waliojifungua

January 3rd, 2024 1 min read

NA FARHIYA HUSSEIN

WAZIRI wa Jinsia na Utamaduni Aisha Jumwa amezindua mradi wa kuwarudisha shule wasichana waliopata mimba za mapema shuleni na wale ambao hawakupata nafasi ya kuendeleza masomo yao kutokana na uchochole. 

Wasichana 10 kutoka sehemu mbalimbali za Kaunti ya Kilifi wamepewa fursa nyingine kwa kurejeshwa shuleni.

Waziri Aisha Jumwa alieleza jinsi alivyopewa nafasi ya pili ya kujikomboa kimaisha na sasa anasema ni wakati wa kurejesha mkono kwa jamii.

Lengo likiwa ni kuwafikia wasichana wengi zaidi ikizingatiwa wapo wengi tu walioacha shule kutokana na mimba za utotoni.

Bi Aisha amedokeza kuwa wizara yake itaanzisha hazina maalumu itakayotumika kuwasaidia wasichana wengi zaidi.

Viongozi waliofika katika mkutano huo akiwemo Mbunge wa Likoni Mishi Mboko wameelezea umuhimu wa hatua ya waziri Jumwa katika jamii.