Equity kutoa huduma kupitia WhatsApp, Facebook, Telegram

Equity kutoa huduma kupitia WhatsApp, Facebook, Telegram

NA MARY WANGARI

BENKI ya Equity imeanzisha mfumo mpya wa utoaji huduma kidijitali katika juhudi za kurahisishia wateja wake mchakato wa kupata huduma za kifedha.

Mfumo huo mpya kwa jina Equity Virtual Assistant (EVA) utawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za benki kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp, Facebook Messenger na Telegram.

Teknolojia hiyo itakayotumika kutoa huduma za benki na usaidizi kwa wateja itawafaidi wateja wa zamani na wale wapya kwa kwa njia ya mawasiliano (chat) na mtumiaji sawia na mawasiliano baina ya marafiki.

Kupitia akaunti zao kwenye mtandao wa EVA, wateja wanaweza kununua vocha ya simu, kutuma hela, kununua bidhaa na huduma, kulipa bili, kutazama salio la pesa pamoja na kupata nakala ya maelezo kuhusu pesa zao wakati wowote popote walipo kupitia mtandao wa kijamii watakaochagua.

Ili kutumia mfumo wa Eva kupitia WhatsApp, hifadhi nambari ya simu 0763000000 katika simu yako na uanze kuwasiliana na EVA au bonyeza https://bit.ly/EquityVirtualAssistant.

Kupitia Facebook Messenger, tafuta EquityEva au bonyeza https://facebook.com/EquityEva.

Iwapo unapendelea Telegramu tafuta @Equitychatbot au bonyeza https://bit.ly/EvaTelegramChatbot

Akitangaza kuhusu teknolojia hiyo mpya katika hafla ya kutoa rasmi matokeo ya robo ya kwanza 2022, Mkurugenzi wa Equity Group, James Mwangi alisema benki hiyo imejitolea kuwekeza katika teknolojia na bidhaa zitakazowapa wateja uhuru zaidi.

“Sisi ni zaidi ya benki, sisi ni wawezeshaji wa mtindo wa maisha, kutimiza mahitaji na matumaini ya wateja na wanajamii wetu. Uzinduzi wa Equity Virtual Assistant, EVA, unaambatana na safari yetu ya kuwezesha huduma na bidhaa zetu kupatikana kidijitali na kimtandao. Tunazidi kuwekeza katika teknolojia na bidhaa zilizoundwa kwa muundo unaowapa wateja wetu uhuru zaidi wa kuchagua, kurahisisha upataji huduma na udhibiti. Kwa kutumia Maarifa Kimitambo, EVA itazidi kukua na kujifunza kutokana na kutangamana na wateja wake ili kutoa majibu. Tunajitahidi kutoa huduma za kifedha kwa wateja wetu popote walipo wakati wowote kwa njia salama, mwafaka na rahisi,” alisema Dkt Mwangi.

You can share this post!

Wawaniaji 16 wa urais wawasilisha saini zao kwa IEBC

Nilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Lamu inakuwa na lami...

T L