Equity yatwaa Benki ya Spire

Equity yatwaa Benki ya Spire

BENKI ya Equity imekamilisha ununuzi wa baadhi ya mali na madeni ya benki ya Spire.

Hii ni baada ya kupokea idhini ya udhibiti kutoka kwa Katibu wa Baraza la Mawaziri Hazina na Mipango chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Benki.Idhini nyingine ni kutoka Benki Kuu ya Kenya, Mamlaka ya Udhibiti wa Vyama vya Ushirika, Mamlaka ya Ushindani ya Kenya, na vibali vya ushirika kutoka kwa bodi na wanahisa wa Benki ya Equity.

Mbali na hayo makubaliano mengi yaliidhinishwa na Mwalimu National Savings & Credit Co -operative Society Limited (Mwalimu Sacco) na benki ya Spire.

Kukamilika kwa ununuzi huo kunatokana na tangazo lililotolewa Septemba 2022 lililoonyesha kwamba iliingia katika miamala na Benki ya Spire kwa mapendekezo ya kupata takriban wateja 20,000.

Wateja hao walio na amana waliwekeza Sh 1.322 bilioni na wateja 3,700 wa mikopo ambao wana salio la mkopo lililoripotiwa.Baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo, wateja walio na amana katika Benki ya Spire, zaidi ya amana zilizosalia kutoka kwa Benki ya Spire, na wateja waliobainishwa wa mkopo sasa watabadilika na kuwa wateja wa Benki ya Equity.

Hii ina maana kwamba wateja hawa watakuwa na akaunti mpya za Benki ya Equity.

Hayo yalisemwa na Dkt James Mwangi, Mkurugenzi Mkuu wa Equity Group aliye kadhalika Mkurugenzi Mtendaji.

  • Tags

You can share this post!

Tume yapendekeza polisi waendelee kuvalia sare za zamani

TSC yasimamisha kazi walimu sita kwa kulazimisha watoto...

T L