Habari Mseto

ERC yawaagiza madereva kuhifadhi risiti za mafuta

June 25th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Waendeshaji wa magari wana kila sababu ya kuweka risiti wanazopata baada ya kununua mafuta kwa magari yao.

Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC) imewashauri kufanya hivyo ili kulisaidia kubuni kesi dhabiti dhidi ya wauzaji wa mafuta machafu nchini.

ERC iliwashauri madereva kuweka jumbe za malipo ya mafuta kwa njia ya simu katika kampeni hiyo.

Tume hiyo ilitoa agizo hilo kutokana na ongezeko la visa vya mafuta machafu nchini kwa kuchanganya dizeli au petroli na mafuta ya taa, kwa lengo la kujipa mapato zaidi.

Waendeshaji wa magari wanafaa kuripoti visa vyovyote vya uharibifu kwa magari yao baada ya kununua mafuta kama vile injini kukosa nguvu au gari kukwama au kutoa moshi usio wa kawaida kwa [email protected] au 0708444000 or 0709336000, ilisema ERC katika notisi.