Erling Haaland aongoza Man-City kupepeta Man-United 6-3 katika gozi la EPL ugani Etihad

Erling Haaland aongoza Man-City kupepeta Man-United 6-3 katika gozi la EPL ugani Etihad

Na MASHIRIKA

NYOTA Erling Haaland, 22, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufunga hat-tricks (mabao matatu katika mechi moja) tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuongoza Manchester City kudhalilisha Manchester United 6-3 ugani Etihad.

Hadi aliposhuka dimbani, fowadi huyo raia wa Norway alikuwa akijivunia hat-tricks nyingine katika ushindi wa 6-0 uliosajiliwa na waajiri wake dhidi ya Nottingham Forest na 4-2 dhidi ya Crystal Palace.

Sasa ana magoli 17 kutokana na mechi 10 ambazo ametandazia Man-City waliomsajili kwa Sh7.3 bilioni kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani muhula huu. Mabao 14 kati ya hayo yametokana na mechi nane za EPL huku matatu yakiwa ya michuano miwili ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Mabao mengine matatu ya Man-City dhidi ya Man-United yalifumwa wavuni na Phil Foden huku wageni wao wakifungiwa na Antony dos Santos na Anthony Martial aliyepata mawili.

Chini ya kocha Pep Guardiola, Man-City sasa wanakamata nafasi ya pili jedwalini kwa alama 20, moja nyuma ya Arsenal wanaoselelea kileleni. Pengo la pointi nane linatamalaki kati ya Man-City na Man-United ambao wana kiu ya kunogesha soka ya UEFA msimu ujao wa 2022-23 chini ya mkufunzi mpya Erik ten Hag.

Ushindi kwa Man-City ugani Etihad ulikuwa wao wa 10 mfululizo katika uga wa nyumbani kwenye mashindano yote ya msimu huu. Mabingwa hao watetezi wanasaka taji la EPL kwa mara ya tatu mfululizo na la tano chini ya Guardiola aliyeanza kudhibiti mikoba yao 2016-17.

Man-City ndio wanajivunia mabao mengi zaidi kutokana na mechi za EPL nyumbani msimu huu. Wamepachika kimiani magoli 20 na kuruhusu wapinzani kutikisa nyavu zao mara sita katika michuano minne iliyopita ya EPL ugani Etihad.

Aidha, wamefunga angalau mabao matatu katika kila mojawapo ya mechi nane zilizopita za EPL ambazo wameshindia nyumbani. Walifunga Man-United jumla ya mabao 6-1 ligini mnamo 2022-23 baada ya kuvuna ushindi wa 4-1 katika mkondo wa pili ugani Etihad.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kylian Mbappe aongoza PSG kupepeta Nice na kudhibiti kilele...

Kilio cha wakazi wa Kariminu vyanzo vya maji safi...

T L