Habari Mseto

Etihad yajizatiti kupunguza hewa chafu

April 8th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Shirika la Ndege la Etihad lilifanikiwa kudhibiti tani 195,000 za hewa chafu mwaka wa 2017.

Hii ni baada ya kuzindua miradi ya kuzuia kutumia mafuta mengi kwa ndege zake. Shirika hilo lilipunguza kiwango cha mafuta kilichotumiwa katika ndege zake kwa zaidi ya tani 62,000 za mafuta.

Kiwango hicho kiliimarisha hatua ya kupunguza matumizi ya mafuta kwa asilimia 3.3 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Kiwango hicho ni sawa na safari 850 za ndege kati ya Abu Dhabi na London, lilisema shirika hilo katika taarifa yake.

Hii ni baada ya shirika hilo kupunguza masaa ya ndege zake hadi 900, hatua iliyopunguza matumizi ya mafuta kwa tani 5,400 na kudhibiti kutolewa kwa tani 17,000 za hewa chafu hewani.

Ili kuwa na athari zaidi, shirika hilo liliondoa ndege ambazo zimekaa sana na kuleta mpya, za kisasa na ambazo hutumia mafuta vizuri Boeing 787.