Michezo

Eto'o amshauri Salah ajiunge na Barca

June 24th, 2019 1 min read

JOHN ASHIHUNDU

PARIS, Ufaransa

Mchezaji nyota, Mohamed Salah wa Liverpool ameshauriwa ajiunge na Barcelona. Ushauri huo umetolewa na mshambuliaji mstaafu, Samuel Eto’o wa Cameoon.

Eto’o alisema hayo, siku cchache tu baada habari kuenea kwamba klabu ya Real Madrid pia inamtafuta staa huyo matata.

“Real Madrid ni timu kubwa, lakini Salah anaweza kung’ara Zaidi iwapo ataamua kujiunga na Barcelona,’ Eto’o aliwaambia waandishi wa habari za michezo.

Eto’o alikuwa na Barcelona kwa kipindi cha miaka mitano, na pia aliwahi kuchezea Real Madrid, mbali na kusakatia klabu za Italia na Urusi kabla ya kujiunga na Liverpool kwa miaka kadhaa.

MKwa sasa mshambuliaji huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 38 anaichezea klabu ya Qatar SC.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea alikuwa miongoni mwa watu Mashuhuri walioshuhudia mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uingereza na Cameroon, Jumapil anaamini Salah ni miongoni mwa wanasoka bora duniani kwa sasa.

“Iwapo atapata fursa ya kuchezea Barcelona, watu watagundua kipaji chake halisi. Mo ana kila kitu cha kumfanya mchezaji bora duniani.”

Salah alisaidia Misri kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mechi yao ya utangulizi ya AFCON dhidi ya Zimbabwe na kesho atakuwa kikosini kuvaana na DR Congo, kabla ya kumalizana na Uganda Jumapili.