Habari Mseto

EU yahamisha afisi zake

November 6th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Ujumbe wa Muungano wa Ulaya (EU) nchini Kenya umehamishia afisi zake kuu Westlands.

Ujumbe huo ulihamishia afisi hizo katika Jumba la Dunhill Towers, katika Barabara ya Waiyaki Way, karibu na kituo cha kibiashara cha Sarit, Oktoba 1.

Kulingana na balozi msaidizi wa ujumbe huo Bw Bruno Pozzi, “EU imekuwa ikitafuta eneo nzuri la afisi zake kwa lengo la kutekeleza mahitaji ya kiusalama, mazingira mema na yanayofaa yaliyo na huduma na maegesho.

Jumba hilo lina orofa 21 ambapo orofa za mwanzo sita ni maegesho, maeneo ya kufanya mazoezi na kuweka jenereta.

Ni jumba la kisasa kwa viwango vyovyote na ndio maana EU ililichagua kuweka afisi zake kwa kuzihamisha kutoka Upper Hill ambako zilikuwa kwa zaidi ya miongo miwili.