Everton yazamisha chombo cha Arsenal katika EPL ugani Goodison Park

Everton yazamisha chombo cha Arsenal katika EPL ugani Goodison Park

Na MASHIRIKA

BAO la dakika za mwisho kutoka kwa fowadi Demarai Gray liliwapa Everton wa 2-1 dhidi ya Arsenal kwenye mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumatatu usiku.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Everton ya kocha Rafael Benitez kusajili kutokana na mechi tisa za awali. Baada ya kupepetwa 4-1 na Liverpool kwenye gozi kali la Merseyside na mkurugenzi wa soka Marcel Brands kuagana nao, Everton walijinyanyua dhidi ya Arsenal na kuendeleza ubabe wao ugani Goodison Park.

Richarlson aliyeshuhudia mabao yake mawili yakikosa kuhesabiwa baada ya teknolojia ya VAR kubainisha kwamba alikuwa ameotea, ndiye alisawazishia Everton katika dakika ya 80 baada ya Arsenal kuwekwa kifua mbele na Martin Odegaard mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Goli la Odegaard lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na Kieran Tierney na Richarlison akapachika kimiani bao lililowavunia ushindi sekunde chache kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa. Ushindi wa Everton uliwapaisha hadi nafasi ya 12 kwenye msimamo wa jedwali la alama 15, nane nyuma ya nambari saba Arsenal.

Iwapo Everton wangeshindwa, basi wangeweka rekodi mbovu zaidi katika historia yao tangu 1994. Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Tierney kuwajibikia Arsenal tangu apate jeraha katikati ya mwezi Oktoba.

You can share this post!

MECHI ZA PATRICK OBOYA CUP: Rongai, Mufya kushiriki fainali

Ujenzi wa Uhuru Park wasimamishwa

T L