FA yapiga Leeds United faini ya Sh3 milioni kwa utovu wa nidhamu

FA yapiga Leeds United faini ya Sh3 milioni kwa utovu wa nidhamu

Na MASHIRIKA

LEEDS United wamepigwa faini ya Sh3 milioni na Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kwa kosa la kutishia usalama wa refa aliyesimamia mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ulioshuhudia Chelsea ikiwapepeta 3-2 mwanzoni mwa Disemba 2021.

Refa Chris Kavanagh aliwapa Chelsea penalti ya pili mwishoni mwa kipindi cha pili baada ya tineja Joe Gelhardt aliyetokea benchi kusawazishia Leeds. Jorginho alipachika wavuni penalti hiyo na kunyima Leeds ya kocha Marcelo Bielsa alama muhimu katika mechi hiyo.

Kichapo hicho kilisaza Leeds na alama sita pekee juu ya mduara wa vikosi vilivyokuwa vikichungulia hatari ya kuteremshwa ngazi mwishoni mwa kampeni za EPL muhula huu. Katika taarifa yake, FA ilisema Leeds walikiri kutowajibika na kuhakikisha kwambe wachezaji wao wanadumisha nidhamu na sifa za uanaspoti mwema.

Walikubali kwamba hatua ya kumzingira refa na kumzomea kulalamikia maamuzi ya Chelsea kupewa penalti ilikiuka sheria. Tangu kukamilika kwa mechi hiyo ugani Stamford Bridge, Leeds wamefungwa mabao 11 katika mechi mbili za EPL na wameteremka hadi nafasi ya 16 kwenye msimamo wa jedwali la EPL.

You can share this post!

Barcelona wapaa hadi nafasi ya saba baada ya kupepeta Elche...

Pigo Arsenal baada ya majeraha na corona kuweka nje mabeki...

T L