NA MARGARET MAINA
BIRINGANYA ina vitamini A na C, ambazo husaidia kulinda seli zako dhidi ya uharibifu.
Pia ina kemikali nyingi za kiasili za mimea ambazo zinaweza kusaidia seli kufanya kazi nzuri zaidi ya usindikaji wa sukari ikiwa una ugonjwa wa kisukari.
Biringanya pia hutumiwa kuandaa mlo tofauti duniani kote.
Ingawa mara nyingi huchukuliwa kuwa mboga, kitaalam ni biringanya ni tunda kwani hukua kutoka kwa mmea wa maua na huwa na mbegu. Aidha biringanya ziko za aina nyingi ambazo zina ukubwa na rangi tofauti.
Faida za kiafya zipatikanazo kwa kula biringanya ni kama vile;
Kupata virutubisho vingi
Biringanya ni chakula chenye virutubisho, kumaanisha kuwa huwa na kiasi kizuri cha vitamini, madini na nyuzi katika kalori chache. Biringanya pia huwa ikiwa ni pamoja na niasini, magnesiamu na shaba.
Kulinda mwili dhidi ya uharibifu
Mbali na kuwa na aina mbalimbali za vitamini na madini, biringanya husaidia kulinda mwili dhidi ya uharibifu unaosababishwa na vitu hatari vinavyojulikana kama radikali. Hivyo husaidia kuzuia aina nyingi za magonjwa sugu kama vile ugonjwa wa moyo.
Kukuza udhibiti wa sukari ya damu
Kuongeza biringanya kwenye lishe yako kunaweza kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Hii ni hasa kwa sababu biringanya zina nyuzinyuzi nyingi, ambazo hupitia mfumo wa usagaji chakula ukiwa mzima.
Nyuzinyuzi zinaweza kupunguza sukari kwenye damu kwa kupunguza kasi ya usagaji chakula na ufyonzwaji wa sukari mwilini. Ufyonzwaji wa polepole huweka viwango vya sukari kwenye damu kuwa sawa.
Inaweza kusaidia kupunguza uzito
Biringanya zina nyuzinyuzi nyingi na kalori chache, na kuzifanya kuwa nyongeza bora kwa lishe yoyote ya kupunguza uzito. Nyuzinyuzi husonga kwenye njia ya utumbo polepole na inaweza kukuza ujazo na shibe hivyo kupunguza ulaji wa kalori. Zaidi ya hayo, biringanya mara nyingi hutumika kama mbadala wa nyuzinyuzi nyingi, zenye kalori ya chini kwa viungo vya kalori ya juu katika mapishi.
Ni rahisi sana kuongeza kwa mlo wako
Biringanya ziko za aina nyingi tena zinapatikana kwa urahisi sana na zinaweza kujumuishwa kwa urahisi katika lishe yako. Biringanya inaweza kuokwa, kuchomwa au kukaangwa na kuliwa kwa kunyunyizia mafuta ya mzeituni au kama kitoweo cha haraka.
Inaweza pia kutumika kama mbadala wa kalori ya chini kwa viungo vingi vya kalori ya juu. Hii inaweza kupunguza ulaji wako wa wanga na kalori, huku ukiongeza nyuzinyuzi na maudhui ya virutubishi kwenye mlo wako.