Habari Mseto

Faini ya Sh70,000 kwa kugonga gari

August 23rd, 2020 1 min read

NA JOSEPH NDUNDA

Dereva wa bodaboda atalazimika kulipa Sh70,ooo baada ya kugonga gari kwenye barabara ya kuu ya Lang’ata  na kuacha abiria wake kwenye eneo la tukio.

Akikosa kulipa faini hiyo atalazimika kufungwa miezi tano jela.

Bw John Mankura alimgonga James Chege Mwangi alipokuwa akiendesha bodaboda kwenye barabara ya Langata Mei 23.

Alishtakiwa kwa kusababisha ajali, kuendesha bodaboda bila leseni na uendeshaji mbaya wa bodaboda.

Mteja wake Saul Nabwela alipata maumivu mengi. Uchunguzi wa polisi ulionyesha kwamba bodaboda  ya Bw Mankura na gari ya Bw Mwangi hazikuwa na shida yeyote hivo ilikuwa ni uendehsji mbaya.

Alikataa mashtaka hayo mbele ya jaji mkuu Abdul Lorot wa korti ya Kibera. Jaji huyo aliamwamuru kulipa Sh50,000 ama kufungwa miezi tatu pia kila kosa alipie Sh10,000 kila moja ama mwezi mmoja jela kila kosa.

 

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA