Familia 100 zakesha kwa baridini baada ya nyumba zao kuchomeka

Familia 100 zakesha kwa baridini baada ya nyumba zao kuchomeka

Na SAMMY KIMATU

NAIROBI

FAMILIA zaidi ya 100 zilikesha nje penye baridi baada ya nyumba zao kuteketea katika kisa cha moto.

Kisa hiki kilitokea katika mtaa wa mabanda wa Kamongo ulioko wodi ya Landi Mawe katika kaunti ndogo ya Starehe.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Bw Meritus Wanjala aliambia Taifa Leo kwamba mali ya thamani isiyojulikana ya pesa iliaribiwa na moto huo.

Aidha, alisema moto ulianzia katika nyumba moja mwendo wa saa nane za mchana kabla ya kuenea kwa nyumba zingine.

Aliongeza kwamba siku mbili kabla ya kisa hiki, nyumba moja nusura iteketee mtoto mchanga akiwa angali ndani ya nyumba peke yake.

“”Mahali hapa kulikuwa na kisa kinginen cha moto amabapo motto mdogo aliwasha kiberiti na kujificha kitandani. Godoro ilisika moto lakinui majirani wakamwokoa, “” Bw Wanjalla akasema.

Kutokana na msongamano wa nyumba, magari ya kuzima moto alilazinmika kusimama katika kampuni moja nayopakana na mtaa huo.

Gari linguine la kuzima moto ilisaidia kupambana na moto ikisimama katika depo ya Kenya Police.

Polisi wanachunguza chanzo cha moto.

  • Tags

You can share this post!

Blue Boys yatwaa ushindi wa KYSD

Mudavadi sasa akimbilia baraka za wazee kabla ya Muhkisa...