Habari Mseto

Familia 45 nje baridini baada ya moto kuteketeza nyumba zao Mukuru-Kayaba

September 25th, 2019 1 min read

Na SAMMY KIMATU

FAMILIA 45 katika eneo la Mandazi Road kwenye mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kayaba ulioko tarafa ya South B, Kaunti ya Nairobi zilikesha nje penye baridi usiku wa kuamkia Jumanne baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba zao.

Inadaiwa moto huo ulianza kutoka ndani ya nyumba moja ambako mwanamke alikuwa akipika chakula akitumia kuni.

Aidha, cheche za moto zilisambaa kwa kasi na kusababisha moto mkubwa huku mama na watoto hao wakikimbilia eneo salama.

Licha ya hakukuwa na majeruhi wala vifo kwenye mkasa huo, mali ya thamani isiyojulikana ilibakia kuwa jivu.

Isitoshe, waporaji hawakuachwa nyuma kupora mali wakijifanya waokoaji na watu wenye moyo wa kutoa huduma za uokozi.

Wakati mmoja vijana waliokuwepo kwenye eneo hilo walipata vitu vinavyohusiana na ushirikina ikiwemo mkanda, pembe na dawa za kienyeji zilizotiwa ndani ya kitambaa na zingine ndani ya pembe hiyo.

Waathiriwa wengine walipigwa na butwaa huku huzuni ikitanda nyusoni mwao wakiwa kimya huku majirani wakijitokeza kuwapa pole.

Kufuatia msongamano wa nyumba baada ya walio na tamaa ya pesa kunyakua bararabara na kujenga nyumba, magari ya kuzima moto kutoka serikali ya Kaunti hayakuwa na budi ila kurudi baada ya kukosa njia.

Vijana washirikiana

Iliwalazimu vijana kushirikiana kuuzima moto huo wakitumia maji ya mifereji na mitungi iliyokuwa na maji kutoka nyumbani huku wengine waking’ang’ana kubomoa nyumba zingine ili kupunguza na kukata moto usienee zaidi.

Waathiriwa wanawaomba wahisani, makampuni, makanisa, serikali na watu binafsi kutoa msaada wowote ili waanze maisha upya.

Kuna msururu na rekodi mbaya ya mtaa huu wa Mukuru-Kaiyaba kuripotiwa visa vya moto tangu miaka ya tisin