Habari Mseto

Familia 800 za Waislamu zapokea chakula kutoka kwa mbunge wa Starehe

June 6th, 2019 1 min read

FAMILIA za Kiislamu zaidi ya 500 zilinufaika kwa msaada wa chakula kutoka kwa mbunge wa Starehe, Bw Charles Njagua Kanyi ‘Jaguar’.

Chakula hicho cha thamani ya Sh2 milioni kilikuwa ni pamoja na mchele, unga wa ngano, mafuta ya kupikia na sukari.

Akiongea kwa niaba ya mbunge huyo, kiongozi wa vijana katika tarafa ya South B, Bw Rodriques Lunalo alisema maudhui ya kupeana chakula yalikuwa ni kuijali jumuiya ya Kiislamu.

“Tumepeana chakula kwa familia 300 hapa Hazina kwa Chifu na familia zingine 500 Ziwani katika wadi ya Kariokor ili tuwajali Waislamu kabla, wakati na baada ya mfungo wa Ramadhani,” Bw Lunalo akasema.