Habari Mseto

Familia ya gavana yapatikana na corona

August 16th, 2020 1 min read

SAMMY LUTTA na FAUSTINE NGILA

Gavana wa Turkana Josphat Nanok amezungumzia jinsi maaMbukizi ya corona yanaendelea kushuMudiwa kaunti hiyo huku familai yake na maafisa wakuu wakipatikana na virusi vya corona.

Bw Nanok alisema kwamba sampuli zilichukuliwa za mkewe, wapishi, watato na walinzi na idara ya afya kuwapima.

Akizungumza kwenye mazishi ya chifu msaidizi Livingston Erupe, gavana huyo alisema kwamba alitumiwa matokeo hayo akipokuwa safarini kuelekea Eldoret kaunti ya Uasin Gishu.

“Virusi vya corona vilitembelea nyumbani kwangu lakini vikajulikana bado zikiwa kwa lango.Nilisafiri matra hio kutoka Eldoret hadi Lowdar na kuagiza kupimwa kwa kila mtu wakiwemo maafisa wamnaofanya kazi afisini mwangu,”alisema.

“Nilithibitisha kwamba maafisa wanaofanya afisini mwangu walipatikana na virusi vya corona.”

Alisema kwamba aliamua kutoa habari hizo kwa umma kwasababu maafisa hao kutangamana na watu wengi.