Habari Mseto

Familia ya JM Kairuki yaomboleza kifo cha mmoja wao

November 9th, 2020 1 min read

JOHN KAMAU NA FAUSTINE NGILA

Familia ya aliyekuwa mwanaisasa maarufu JM Kariuki inaomboleza kifo cha mwanawe aliyekuwa mbuge wa Nyandarua Kasakzini Tony Kariuki aliyefariki Jumapili.

Habari za kufariki kwake zilitolewa na dada yake mtandaoni Jumapili jioni Jane Kariuki: “Tony siamini kwamba umetuacha,”aliandika.

Kabla ya kifo chake alikuwa anaendesha kampuni ambaye ndiye aliyekuwa mkurugenzi mkuu pia alikuwa mkurugenzi mkuu wa JM Kariuki Foundation for Peace, Leadership and Transitional Governance.

Tony ambaye alihitimu kutka chuo kikuu cha Maryland mwaka wa 1995 alifanya kazi kwa kampuni tofauti Marekani kabla ya kurejea nyumbani.

Kinyume na baba yake Tony hakuwa mwanasiasa.

JM Kariuki alikuwwa mbunge wa Nyandarua Kasakzini ambaye kifo chake kilichotokea 1975 na kuzua maandamano ambapo ilikisiwa kilitokana na maafisa wakuu serikalini.