Habari Mseto

Familia ya muuguzi wa Homa Bay yataka ifidiwe

August 7th, 2020 1 min read

NA GEORGE ODIWUOR NA FAUSTINE NGILA

Marafiki wa muuguzi wa Homa Bay Marian Awuor Adumbo aliyefariki kutokana na virusi vya corona wiki iliyopita waliomba kufidiwa kwa familia hiyo katika mazishi yaliyofanyika Ijumaa.

Awuor aliyekuwa muuguzi wa upasuaji alifariki akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kisii Agosti 2.

Wafanyakazi wenzake walisema kwamba serikali inapaswa kuwalipa watu wa familia hiyo kw asababu inahusika na kifo chake.

Familia ya Awuor imeilaumu hospitali ya Kisii aliyokuwa akifanyia kazi ya Rachuonyi kwa kutomjali.