Habari Mseto

Familia yalia mwili wa mwanao kukosekana mochari

November 13th, 2020 1 min read

IRENE MUGO NA FAUSTINE NGILA

Baada ya wiki moja ya kuomboleza, familia moja eneo la Othaya imelazimika kuahirisha mazishi ya mwana wao baada ya mwili wake kukosekana kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Outspan.

Mamia ya waombolezaji walikuwa wamekusanyika kwenye chumba hicho cha maiti kukusanya mwili Jumanne ili wausafirishe kwenye Kijiji cha Gaturuturu.

Mwili wa Bi Monicah Mumbi wa mika 77 ulipelekwachumbani huko wiki iliyopita ukigoja kuzikwa Jumanne.

Waombolezaji walishangaa wakati muhudumu wa chuba hicho alipowapata mwili ambao hawangeweza kuutambua.

Familia hiyo ilishangaa kwani mwwili hio ilikuwa na mwonekano tofauti huku wakisema kwamba jamaa yao alikuwa na nywele nyeupe na meno iliyogoka.

Bi Loise Wangari mwanawe mwendazake alisema kwamba walikataa mwili huo.

“Mama uangu alikuwa natumia meno ya kubandika kwani hakuwa na meno na meno hayo yaliachwa nyumbani wakati alipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti .Miili waliokuwa wakitupa ilikuwa na mweno yote hivo tungekubali aje?”alisema Bi Wangari.