Habari Mseto

Familia yasaka mwana aliyepotea huku watu wasiojulikana wakidai ada ya kumkomboa

June 11th, 2024 1 min read

NA DOMNIC OMBOK

FAMILIA moja mjini Kisumu inamtafuta mtoto wao wa kiume aliyetoweka Mei 21, huku wakipokea simu kutoka kwa watu wasiowafahamu wakidai malipo.

Bw Chrysantus Amimo, 33, alimaliza masomo yake katika Kisumu National Polytechnic mwaka wa 2015, na kuwa mkulima.

Mamake, Bi Euphemia Atieno, alisema walianza kupatwa na wasiwasi alipokosa kurejea nyumbani.

Aliripoti katika Kituo cha Polisi cha Nyangeta huko Kibos.

“Mwanangu hatoki nyumbani bila kutujulisha, na hakosi chakula cha mchana,” alisema Bi Atieno.

Familia yake ilianza kusambaza mabango kwenye mitandao ya kijamii na wakiwa na tumaini la kumpata.

Babake, Bw Lazarus Abungu alifichua kupokea simu za kutatanisha kwa watu wasiofahamika, kila mmoja akidai kumwona.

“Tumepokea simu za kutatanisha baada ya kuchapisha, wakidai fidia,” alifichua Bw Abungu.