Habari Mseto

Familia yataka haki baada ya msichana kubakwa na kukatwa nyeti zake

January 7th, 2019 1 min read

Na George Odiwuor

FAMILIA moja mjini Homa Bay, inatafuta haki kwa msichana wao mwenye umri wa miaka 13 aliyebakwa na wanaume wawili ambao pia walikata sehemu yake nyeti kwa kutumia wembe.

Msichana huyo wa darasa la nane katika shule moja ya msingi mjni humo, alipatwa na madhila hayo baada ya stima kupotea na giza totoro kutanda. Wanaume hao walitumiafursa hiyo kumdhulumu.

Tukio hilo lisilo la kawaida limewaacha wanakijiji wa mtaa wa Shauri yako ambako msichana huyo na familia yake huishi kwa mshtuko na mshangao mkubwa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi kaunti ya Homabay Marius Tum, alisema kwamba maafisa wake wamewanasa washukiwa wawili wanaohusishwa na kitendo hicho cha uhayawani.