Habari Mseto

Fazul abana sababu ya kujiuzulu

March 2nd, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Fazul Muhamed, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali alitangaza kujiuzulu Jumatatu baada ya mahakama kuzuia kwa muda kandarasi mpya kwake.

Katika notisi ya kujiuzulu, Mahamed hakueleza sababu kamili ya kujiuzulu, na badala yake kushukuru bodi ya shirika hilo.

Alisema ataondoka afisini Aprili 30, baada ya kuhudumu katika shirika hilo katika muda wa miaka mitatu.

Katika barua hiyo ya kujiuzulu iliyoandikwa Februari 19, Mahamed alisema , “Kwa muda wa miaka mitatu, nimehudumu kwa furaha kubwa na msisimko.”

Bw Mahamed alikuwa akikabiliwa na shutuma nyingi hasa kutoka kwa upinzani na mashirika ya kijamii kwa kubatilisha usajili wa baadhi ya mashirika.

Pia, kiwango chake cha elimu kilikuwa kimetiliwa shaka baada ya Chuo Kikuu cha Egerton kukana kuwa alihitimu digrii kutoka humo.