Habari

Feisal Abdallah Bader aibuka mshindi wa kiti cha ubunge Msambweni

December 16th, 2020 1 min read

Na MOHAMED AHMED

MGOMBEA wa kujitegemea Salim, Feisal Abdallah Bader ameibuka mshindi wa kiti cha ubunge Msambweni kwa kujizolea kura 15,251 mpinzani wake wa karibu katika uchaguzi mdogo wa Jumanne, Boga Omari Idd wa ODM akipata kura 10,444.

Afisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC Yusuf Abubakar amemtangaza rasmi Bw Bader kuwa ndiye mshindi.

Wagombea wengine walikuwa ni Abdulrahman, Sheikh Mahamoud aliyepata kura 790, Wamwachai, Marere Mwarapayo (300) akipeperusha bendera ya Wiper, Liganje Khamis Mwakaonje (230), Bilali Charles Bambo (135), Mwakulonda Ali Hassani (107), Kumaka Mansury Abdurahamani (38) na Onyango Sharlet Akinyi aliyemaliza wa mwisho kwa kuridhika na kura 18 pekee.

Hii ni baada ya kukamilika kuhesabiwa kwa kura halali zilizotumbukizwa katika maboksi na wapigakura wa eneobunge hilo.

Idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 39.58 ya jumla ya wapigakura 69,003 waliojisajili.

Kiti hicho kiliachwa wazi baada ya kifo cha Suleiman Dori.