Fernandinho arejea Brazil kuchezea Athletico Paranaense baada ya kuondoka Man-City

Fernandinho arejea Brazil kuchezea Athletico Paranaense baada ya kuondoka Man-City

Na MASHIRIKA

KIUNGO mkabaji na nahodha wa zamani wa Manchester City, Fernandinho Luiz Roza, 37, amejiunga upya na kikosi cha Athletico Paranaense kilichompokeza malezi ya awali kabisa kwenye ulingo wa soka nchini Brazil.

Kwa mujibu wa Fernandinho aliyekuwa akiwaniwa na vikosi kadhaa ndani na nje ya bara Ulaya, “kuvalia tena jezi za Paranaense kutamridhisha zaidi”.

Aliondoka kambini mwa Man-City mwishoni mwa msimu wa 2021-22 baada ya kuhumu ugani Etihad kwa kipindi cha miaka tisa.

Sogora huyo anayejivunia kushindia Man-City mataji matano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) anarejea Paranaense miaka 17 baada ya kuagana na kikosi hicho na kuyoyomea Ukraine kuchezea Shakhtar Donetsk.

Paranaense kwa sasa wananolewa na kocha wa zamani wa Chelsea, Luiz Felipe Scolari.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Ruto asema hana shida na maafisa wa IEBC

Mjukuu wa Moi aandamwa na mke waliyetalikiana agharimie...

T L