Michezo

Fifa yaruhusu timu kuanza mapema usajili wa wachezaji wapya

June 13th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

ZURICH, Uswisi

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limeruhusu timu kuanza shughuli za kusajili wachezaji wapya hata kabla ya msimu huu wa 2019/20 kumalizika.

Msimu ulisimamishwa ghafla mwezi Machi kutokana na janga la Covid-19, na kuvuruga kalenda za mashirikisho ya soka kote ulimwenguni.

Mikataba ya wachezaji wengi inatarajiwa kumalizika mwezi huu wa Juni, ambapo baadhi yao watakuwa huru kujiunga na timu zingine kabla ya msimu kumalizika.

Hata hivyo, baada ya kufanya makubaliano na wachezaji hao wapya, timu zimeshauriwa kusubiri hadi msimu huishe ndipo wajiunge rasmi na timu zao.

“Ili kusitokee kukosekana kwa baadhi yao kupata klabu wanazotaka, wachezaji wamekubaliwa kufanya mikataba na klabu tatu wakati wakiendelea kuchezea klabu zao za sasa hadi msimu umalizike.