Firat akaribia kurejea kushika usukani Kenya

Firat akaribia kurejea kushika usukani Kenya

NA JOHN ASHIHUNDU

KOCHA Engin Firat anatarajiwa kurejea usukani kama kocha mkuu wa Harambee Stars, hii ikiwa mara ya pili kwa raia huyo wa Uturuki kupewa jukumu hilo.

Firat aliondoka ghafla Novembe mwaka uliopita, wakati Kenya ikikaribia kupigwa marufuku na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).

Alikuwa ameajiriwa kwa mkataba wa miaka miwili na Shirikisho la Soka Nchini (FKF) kusimamia mechi mbili za mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia kuelekea fainali za Qatar 2022.

Lakini katika mechi hizo mchujo, Kenya ilichapwa 6-0 na Mali, kabla ya kushindwa 2-0 katika mechi nyingine iliyochezewa Nyayo Stadium.

“Katika mkutano wetu, ilipendekezwa Firat amepewe mkataba wa kunoa Harambee Stars, lakini ni pendekezo tu ambalo lazima liidhinishwe rasmi. Ilisemekana Stars walicheza vizuri wakati akiwa usukani,” mtu mmoja aliyehudhuria kikao hicho alisema.

Hii imejiri soku moja tu baada ya kocha huyo kudai kwamba alifurahia maisha alipokuwa hapa nchini, na kwamba angependa kuendelea.

“Tatizo pekee nchini Kenya ni ukosefu wa vifaa vinavyofaa, mbali na viwanja vya hali duni, changamoto ambalo ni kuu barani Afrika. Lakini kuandaa Harambee Stars ni kazi ningependa nipewe kwa mara nyingine. Safari ni ndefu, lakini ningependa nipewe nafasi tena.”

Kenya ilirejeshwa katika mashindano ya kimataifa Jumatatu, lakini haijakubaliwa kushiriki katika mchujo wa kuwania nafasi ya kushiriki AFCON, zilizoanza kabla ya Kenya kuadhibiwa. Hivyo, Kenya itakuwa nje ya mashindano ya kimataifa hadi 2024.

Kocha Firat anamiliki cheti cha UEFA Pro, na majuzi alikaribia kuteuliwa kama kocha wa timu ya taifa ya Moldova.

Klabu za Saipa, Folad Tabriz na Sepahan pamoja na timu ya taifa ya Iran ni miongoni mwa alizowahi kunoa.

  • Tags

You can share this post!

Waziri Namwamba atoa onyo kali baada ya Kenya kuondolewa...

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Korea Kusini sasa kutoana jasho...

T L