Michezo

Flash ndiye bingwa wa mbio za magari 2018

June 11th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Carl ‘Flash’ Tundo amerukia uongozi wa mashindano ya Kenya ya mbio za magari (KNRC) mwaka 2018 baada ya kutwaa taji la raundi ya nne mjini Athi River, Juni 9, 2018.

Tundo alijizolea alama 25 katika duru hiyo na kuimarisha alama zake hadi 75. Allingia duru ya nne akiwa katika nafasi ya pili. Ameng’oa Baldev Chager kileleni. Chager, ambaye alikamilisha shughuli ya Athi River katika nafasi ya tatu, ana alama 71. Duru ya tano itfanyika wikendi ya Julai 7-8.

Matokeo ya KNRC ya duru ya nne (10-bora): Carl Tundo/Tim Jessop (Mitsubishi EvoX) dakika 84.44, Manvir Baryan/Drew Sturrock (Skoda Fabia) 85.18, Baldev Chager/Ravi Soni (Mitsubishi EvoX) 85.34, Onkar Rai/Gavin Laurence (Skoda Fabia) 85.54,

Eric Bengi/Tuta Mionki (Subaru Impreza) 89.41, Jasmeet Chana/Ravi Chana (Mitsubishi EvoX) 92.51, Farhaaz Khan/Keith Henrie (Mitsubishi EvoX) 93.06, Ammar Haq/Victor Okundi (Mitsubishi EvoX) 98.32, Nikhil Sachania/Alfir Khan (Mitsubishi EvoX) 103.59, Aakif Virani/Azhar Bhatti (Subaru Impreza) 107.36.