Fuliza ya Safaricom kuwezesha wasio na hela kuzituma kupitia M-Pesa

Fuliza ya Safaricom kuwezesha wasio na hela kuzituma kupitia M-Pesa

Na BERNARDINE MUTANU

WATUMIZI wa M-Pesa sasa wanaweza kununua bidhaa au kutuma pesa wakiwa hawana pesa katika akaunti zao za simu.

Hii ni baada ya Safaricom kuzindua mpango wa Fuliza kwa watumiaji wote wa M-Pesa nchini.

Jumamosi, Safaricom ilituma jumbe kwa wateja wake kuwafahamisha kuhusiana na huduma hiyo mpya.

Safaricom iliamua kuanzisha mpango huo baada ya kuufanyia majaribio Novemba mwaka 2018.

Watumiaji wa M-Pesa nchini ni 24.2 milioni na wanatarajiwa kunufaishwa na mradi huo.

M-Pesa imekuwa ikifanya vyema huku ikiwa imepata faida ya asilimia 20.22 katika nusu ya pili ya mwaka jana ambapo ilipata faida ya Sh31.5 bilioni.

Kwa kutumia Fuliza, wateja watakuwa na uwezo wa kutumia hadi Sh50, 000 kulingana na kiwango wanachohitaji.

Kampuni hiyo inashirikiana na Benki ya KCB na CBA. Mteja akichukua, atalipa kwa riba ya asilimia 0.5 kwa siku.

You can share this post!

Tamko la ‘Washenzi’ lilivyowakera wapigakura wa...

St Georges ya Ethiopia yaongezea hela kupata huduma za Mieno

adminleo