FUNGUKA: ‘Kijogoo mtaani, sichoki kuwika’

FUNGUKA: ‘Kijogoo mtaani, sichoki kuwika’

Na PAULINE ONGAJI

ROBA kama anavyofahamika na wenzake, ni mwanafunzi katika chuo kikuu kimoja jijini Nairobi.

Ukimtazama mwanamume huyu wa miaka 22, utadhani kuwa ni kijana wa kawaida anayezama masomoni. Mbali na kuendelea kuzoa alama nzuri chuoni, uhusiano wake na wanafunzi wenzake ni mzuri huku wahadhiri wakimtambua kutokana na werevu wake.

Lakini usipumbazwe na picha hii nzuri anayoonyesha watu. Kaka huyu ameficha maovu tele. Kwanza Roba ni mjanja ajabu. Hasa katika masuala ya mahaba, amebobea kiasi kwamba ni wachache wanaoepuka mtego wake kila anaporusha mistari.

Kinachoshangaza pia ni kwamba hana mipaka. Anarusha kokote na popote pasipo ubaguzi wa mwonekano, umri au tabaka. Kiu yake ya mapenzi inazimwa na yeyote yule mradi amevalia rinda.

Mtaani yeye ni kijogoo cha kuwapa burudani wake za watu ambapo ashiki hazimpi hata nafasi ya subira angalau kukodisha chumba.

Iwe nyumbani kwa mwanamke, kichakani au chumbani, kwa Roba, mahali popote pale panatosha kumalizia haja yake na hana majuto ya kufanya anachofurahia.

“Mimi ni msamaria mwema na nia yangu ya kufanya hivi ni kutokana na huruma ninayo kwa wanawake hawa ambao mara nyingi hulalamika kupuuzwa na wenzao kwenye ndoa.

Nia yangu ni njema kwani siitishi pesa na mradi nimemhudumia binti, sina haja na uhusiano wa kudumu. Tukimaliza shughuli, kila mtu ashika hamsini zake.

Mabinti wengi ninaoburudisha hurudi tena na tena kwa sababu hakuna mwunganisho nao na situmai kunufaika na chochote.

Sina gharama na haja ni kuhakikisha kuwa wanawake hawa wanashughulikiwa vilivyo badala ya kusaka huduma hizi kwingine. Ajabu ni kwamba sichoki, naweza wika mchana kutwa endapo siendi chuoni.

Kinachoshangaza ni kwamba nimedumisha uhusiano mzuri na waume za hawa wanawake na sidhani kati yao kuna hata mmoja anayeshuku nachovya buyu lao.

Nilianza kufanya hivi miaka kumi iliyopita baada ya kuwasili jijini Nairobi ambapo nilijiunga na chuo kikuu kimoja. Kutokana na sababu kuwa nilikuwa nahudhuria masomo wakati wa jioni, hapa ndipo wazo la kuwahudumia mabibi wanaobaki nyumbani liliponijia kwani nyakati za asubuhi nilikuwa napisha muda tu.

Tofauti na baadhi ya wanaume wenzangu wanaotumia “chombo” hiki kama kitega uchumi, kwangu hiki ni kifaa cha kuwaokoa wanaoachwa hoi na wenzao chumbani. Nimebobea katika masuala haya kiasi kuwa kwa miaka hii yote sijawahi fumaniwa na vipusa ninaohudumia kwani najua ratiba zao kamili.

Kwa ufupi, mimi kama Roba nimeumbwa kufurahia kwichi kwichi bila haya. Kwa hivyo kwa nini nimnyime binti ilhali matumizi ya chombo hiki hayatapunguza urefu wake? Kwa nini niwanyime binadamu wenzangu uhondo wa chakula hiki ambacho mwishowe kitaliwa na mchwa?”

You can share this post!

CHOCHEO: Utachombeza au kuyatema Valentino hii?

MWANAMUME KAMILI: Ole nyinyi mliosikiliza na kusadiki...