FUNGUKA: Msisimko wangu wa mahaba hutokana na kutazama panya!

FUNGUKA: Msisimko wangu wa mahaba hutokana na kutazama panya!

NA PAULINE ONGAJI

Katika ulimwengu huu wa mambo tofauti, bila shaka hata binadamu hakuna anayefanana na mwenziwe, iwe kimaumbile au kitabia. Pia katika masuala ya mahaba, vichocheo vyetu havifanani.

Kuna wale wanaofurahia mguso. Kuna wale ambao hisia zao huchochewa wanaponong’onezewa maneno matamu masikioni na kuna wengine ambao wanachotazama huwasisimua wakati wa mahaba.

Kwake Eric, hisia zake za mahaba huchochewa na mambo yasiyo ya kawaida, angaa kulingana na baadhi ya watu wanaomfahamu. Kaka huyu hupata msisimko kwa kuwatazama panya.

Eric ni kaka wa miaka 39 na ni afisa mkuu katika idara ya fedha katika shirika moja la kimataifa jijini Nairobi. Kazi hii ya haiba ya juu ina kipato kikubwa, na ni kupitia fedha hizi ambapo amewekeza katika biashara mbalimbali. Pia, amejenga nyumba kadhaa za kupangisha na anamiliki magari kadha wa kadha.

Kimaumbile, Mungu alikuwa mkarimu kwake. Ni mtanashati ajabu ambapo ni kawaida kuona mabinti wakimpa tabasamu za kishua kazini na anapotembea barabarani.

Mbali na utanashati huu, kaka huyu ni bingwa katika masuala ya mahaba na inasemekana kwa wale ashawahi waonja, hurejea tena na tena. Lakini uzuri huu usikupumbaze. Ikiwa unataka kuufurahia, basi uwe tayari kustahimili kichocheo chake cha mahaba kisicho cha kawaida, kama anavyosimulia.

“Kwa kawaida mimi hupata msisimko ninapotazama panya wakati wa mahaba. Sio panya mmoja. Nazungumzia panya kumi au zaidi walio hai.

Ashiki yangu haichochewi kwa kutazama wakiwa wamesimama tu, wakiwa wamelala au wakiwa wamekufa, bali wakiwa wanazunguka huku na kule.Pengine utauliza nini kuhusu wanyama hawa kinachonifurahisha? Ile sauti yao wakilia, au tabia yao ya kunusanusa vitu na kurukaruka huku na kule, ni kichocheo tosha kwangu.

Mimi hufurahia sana kiasi kwamba hutamani wapate nafasi ya kuungana nasi kitandani.Kwa hivyo kabla ya kunivutia, lazima uwe tayari kuonyesha kwamba huwaogopi viumbe hawa.

Ikiwa wewe ni binti unayepiga mayowe ukiwaona panya, basi tafadhali tafuta kwingineko. Katika miadi yetu ya kwanza nitawaleta wanyama hawa na lazima uwaguse.

Huo ndio mtihani wa kwanza.Ndiposa katika ua la jumba langu utawapata panya wametapakaa kila mahali. Aidha, katika jumba langu nimehifadhi chumba kimoja kinachowekwa masalio ya chakula; mazingira mwafaka ya wanyama hawa.

Sio tu chumbani, hata kwenye bafu lazima wanyama hawa waungane nami nikioga. Mezani, lazima wawe nami ambapo nikila, nao wanarukaruka huku na kule karibu yangu.

Ukijaribu kuwafukuza, basi huo ndio mwisho kati yangu nawe.Yeyote anayestahimili na kukubali masharti yangu, basi namhakikishia uhondo wa kipekee.

Ndiposa licha ya masharti haya ambayo kwa wengine ni ya kutisha, mabinti wanaopata fursa ya kuburudishwa nami kwa kawaida hawataki kuniacha.

Sijawahi kuwa na mchumba kwa kipindi kisichopungua miaka mitano, na mara nyingi ni mimi ndiye huwatema. Hata sasa kuna mabinti watatu wanaonibembeleza tufunge ndoa”.

You can share this post!

FATAKI: Imarisha chombo chako uweze kupiga mbizi baharini...

Utata wa uteuzi wa Mwende Mwinzi waendelea kutokota