FUNGUKA: ‘Nacheza mechi za majuu pekee’

FUNGUKA: ‘Nacheza mechi za majuu pekee’

Na PAULINE ONGAJI

KWA wengi suala la mahusiano ya pembeni katika ndoa haliruhusiwi kamwe.

Lakini licha ya haya, kuna baadhi ya wanaume ambao bado wana mwanya wa kurambaramba vya nje.

Daniel ni mmoja wao. Inapowadia katika masuala ya kusakata mechi za nje, yeye ni gwiji. Dume hili haliitwi gwiji tu bila sababu kwani viwango vyalo vya kusakata mechi za nje, ni vya kipekee.

Daniel ana mke, na pamoja na mkewe wamejaliwa watoto watatu. Yeye ni mfanyabiashara shupavu ambapo anamiliki majengo kadhaa ya kibiashara jijini Nairobi na Mombasa. Kwa upande mwingine, mkewe ni meneja wa benki moja jijini Nairobi.

Mbali na kuumbika kwelikweli, kaka huyu ana mapeni si haba. Biashara zake zinampa mapato mazuri na pamoja na mkewe, wanajiweza kifedha.

Hii inamaanisha kwamba hana tatizo lolote la kifedha na hakuna wakati hata mmoja ambapo familia yao imeonekana kupungukiwa.

Machoni mwa wenzake Daniel ana kila kitu anachohitaji maishani. Sio tu pesa na sifa, bali pia mke mrembo na watoto maridadi. Lakini licha ya haya, ameshindwa kabisa kuachana na mechi za ugenini. Hasa huwalenga wanawake wenye mifuko mizito na mara nyingi shughuli zake huzitekeleza kimataifa.

“Mechi zangu huchezwa katika miji ya nchi za ng’ambo kama vile London, Paris, New York, kwa kutaja tu michache. Kwa kawaida mimi hunasa mabinti wenye mifuko mizito, kumaanisha kwamba wana uwezo wa kifedha wa kugharimia ziara zetu.

Mimi hunasa wanawake mabwenyenye mtandaoni na kuwashawishi kufadhili hizo ziara zangu, vile vile kuishi katika baadhi ya hoteli ghali sana ulimwenguni.

Nina mpenzi katika sehemu kadha duniani, na sio tu wapenzi, mabinti walio na akaunti kubwa kubwa za pesa.

Nina mpenzi kutoka Uswisi niliyekutana naye mtandaoni na baada ya kufanya uchunguzi nilitambua kuwa ana hisa katika kampuni kubwa ya kuunda magari. Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa mtandaoni alinitumia tikiti ya ndege kwenda jijini Zurich. Huko tulikaa kwa wiki kadhaa na kuzuru sehemu kadha wa kadha nchini humo.

Tukiwa nchini humo nilipata fursa ya kukutana na milionea fulani kutoka Ujerumani ambapo alionekana kuvutiwa nami. Tulipokuwa tumekaa kwenye ukumbi wa hoteli pamoja na huyo mpenzi wangu raia wa Uswisi, niligundua kwamba binti huyo Mjerumani alikuwa akinikodolea macho kwa muda. Mswisi alipoondoka kwenda msalani, binti hakupoteza muda na kuniitisha namba ya simu.

Licha ya kuwa nina pesa zangu, binti huyo Mswisi amekuwa akinitumia kitita kikubwa cha pesa kila mwisho wa mwezi. Anafahamu kwamba nina mke na watoto, lakini hilo halimbabaishi. Hata anapotuma pesa, anahakikisha kwamba anamtumia pia mke wangu.

Pia, nina binti fulani kutoka Amerika ambaye tulikutana naye jijini Nairobi tukiwa katika kongamano la kibiashara. Kwa muda sasa amekuwa akifadhili ziara zetu katika miji mikuu kadha wa kadha duniani”.

Mke wangu anajua kuhusu maisha yangu haya ya pembeni na hana tatizo mradi niwe mwangalifu na kujikinga kutokana na maradhi ya zinaa. Anajua kwamba yeye pia hunufaika kifedha kutokana na mahusiano yangu haya”.

 

You can share this post!

MWANAMUME KAMILI: Kama lazima kumla mtu jamani msile muda...

CHOCHEO: Chunga ‘mboch’ asijepasha joto kitanda chako