FUNGUKA: ‘Najua mtasema ni wazimu…!’

FUNGUKA: ‘Najua mtasema ni wazimu…!’

Na PAULINE ONGAJI

KATIKA masuala ya mahaba, watu wamejulikana kujihusisha na mambo tofauti ili kushibisha kiu yao ya mapenzi.

Mengine sio ya kawaida.

Jackie ni mmoja wao. Kwa miaka, binti huyu amekuwa akijihusisha na tendo la kushangaza kama mbinu ya kuchochea ashiki nyumbani kwake. Anasisimuliwa na madume wanaovalia chupi za mabinti.

Jackie ana umri wa miaka 39 na anafanya kazi kama mkurugenzi wa taasisi moja kubwa jijini Mombasa. Ni kazi aliyopata baada ya kuhitimu chuoni mwongo mmoja unusu uliopita ambapo alifanya vyema sana alipokuwa anasomea shahada yake.

Akiwa katika shule za msingi na upili, alikuwa mmoja wa wanafunzi werevu zaidi, suala lililomhifadhia nafasi katika chuo kikuu kimoja hapa nchini.

Ustadi wake kimasomo, pia ulimnasia nafasi ya ufadhili wa kimasomo, kusomea shahada ya uzamili katika chuo kikuu kimoja nchini Uingereza.

Lakini kando na masuala ya kimasomo, ameumbwa akaumbika huku urembo wake ukiwa kivutio cha madume wengi wanaopata fursa ya kukutana naye.

Lakini licha ya sifa hizi zote, Jackie anakabiliwa na tatizo moja. Hawezi kamwe kuhifadhi mahusiano ya kimapenzi, suala linalotokana na tabia yake isiyo ya kawaida, kama anavyoeleza zaidi.

“Nafurahia mwanamume anayevalia chupi za mabinti. Ikiwa unataka kuwa mpenzi, mchumba na hatimaye mume wangu, unapaswa kuelewa kwamba mwanamume asiyevalia mavazi haya ni kero kwangu.

Hii inamaanisha kwamba, kama mpenzi au mume wangu, unapaswa kukubali kwamba pindi tunapoanza uchumba na hatimaye kufunga ndoa, basi uwe tayari kuvalia chupi hizi hasa tukiwa pamoja.

Pindi unapoingia nyumbani kutoka kazini, basi nguo zako zote unazivua na kusalia na hayo mavazi. Nikikuandalia chakula, uwe umevalia sio tu chupi, bali pia kamisi na mavazi mengine ya ndani yanayovaliwa na wanawake. Hii huniongezea ashiki, na hivyo kuongeza uhondo tunapoanza mahaba.

Suala la mwonekano sio tatizo, uwe na kitambi au kifua kipana, hilo halinibabaishi mradi uwe tayari kukumbatia matakwa yangu.

Kumbuka kwamba ikiwa hauna hayo mavazi niko tayari kukununulia kila ninapoenda dukani kununua zangu.

Lakini kuna masharti pia ambayo lazima yafuatwe. Kwa mfano, kaka adumishe usafi, kumaanisha pindi unapoingia nyumbani kutoka kazini au shughuli hizo zingine, lazima uoge, ubadilishe mavazi mengine na kujipuulizia marashi.

Nimethibitisha mara kadhaa kwamba kila mwenzangu anapokosa kuzingatia haya, penzi langu kwake hutoweka. Ni suala ambalo limeninyima fursa kadhaa za kuolewa kwani kila ninapokutana na kaka na kumpa masharti haya, anayafuata kwa muda, lakini baadaye anashindwa na kujitoa.

Hata hivyo nina matumaini ya kwamba katika harakati hizi za kumtafuta mume atakayekumbatia masharti yangu, hatimaye nitafanikiwa”.

You can share this post!

Kiwanda cha mananasi kujengwa Gatundu Kaskazini

CHOCHEO: Siri ya mapenzi yenye raha na yanayodumu