Makala

FUNGUKA: 'Namtafuna na simpi hata senti'

October 5th, 2019 2 min read

Na PAULINE ONGAJI

UNAPOMTAZAMA Muna ni rahisi kudhania kuwa ni mtu anayeheshimika katika jamii.

Kwanza ana kazi nzuri katika mojawapo ya vyombo tajika vya habari nchini.

Mbali na hayo ni mtu anayezingatia dini. Ana wake wawili ambapo yuko sawa kulingana na viwango vya dini yake inayomruhusu kuwa na wake hadi kufikia wanne.

Pamoja na wake zake hao wawili, wamejaliwa watoto saba na japo hawana ajira, mshahara mzuri unamwezesha kushughulikia familia yake bila tatizo.

Pengine utadhani kwamba basi na familia hii, Muna anapaswa kuwa mtulivu, lakini mambo sio hivyo.

Bwana huyu ana tabia mbovu. Licha ya kuwa na wake wawili, yaonekana kana kwamba hatosheki na mahaba chumbani.

Kwa hivyo amebuni mbinu zingine za kushibisha kiu hii.

Hasa anapenda makahaba, na hivyo kila usiku hasa wikendi utampata ameegesha gari lake katika mojawapo ya barabara zinazojulikana kutawaliwa na mabinti hao.

Sio hayo tu! Bwana huyu ana mazoea ya kuramba na kutoweka bila kulipia huduma anazopokea.

“Siwezi kulipia kunywa maji ya kisima ambacho sio wewe mwenyewe uliyechimba, na hivyo mimi huenda kupokea huduma vilivyo na kudinda kulipa bila majuto.

Kutokana na gari langu kubwa, mabinti hung’ang’ana kunihudumia wanapoliona limeegeshwa. Kwa hivyo ukiingia kwenye gari langu, nakupeleka katika chumba cha hoteli ambapo tunakubaliana malipo kisha unanihudumia.

Ujanja wangu ni kwamba mimi uahidi hao mabinti kwamba nitawalipa pesa nyingi, pesa ambazo mimi hutoa na hata kuziweka kwenye meza. Hii hunihakikishia kwamba napokea huduma bora kabisa. Lakini ukishamaliza tu, nachukua senti zangu na kuziweka mfukoni kabla ya kukufurusha nje.

Mara kwa mara nimekumbana na mabinti wanaozua vurugu baada ya hapo ila nimefanya haya kwa miaka mingi na hivyo najulikana katika lojingi nyingi ambapo binti akijaribu kuleta fujo ni yeye atakayerushwa nje.

Isitoshe, nawafahamu maafisa wengi wa polisi jijini ambapo hata ukijaribu kunishtaki, ni wewe utatupwa korokoroni.

Nakumbuka wakati mmoja kuna binti aliyenianika mtandaoni na hata kuonyesha juisi tuliyokunywa tukiwa chumbani kama ushahidi, lakini hilo halikunibabaisha.

Nafahamika katika sehemu hizi kwani nimezoea kiasi kwamba hata hao mabinti wanaponiona, wanaangua kicheko wakijua kwamba atakayejitolea kunitumbuiza hatolipwa hata kipeni.

Nafanya hivi kwani kwa muda mrefu mabinti wamekuwa wakinufaika kutokana na chombo ambacho sio wao wenyewe walikiumba, na hiyo sio haki. Bila shaka sio kwamba umlazimishe au umbake binti ya wenyewe. Tumia mistari yako kupata unachotaka kisha usepe.

Sasa nafikiria kupeleka ujanja wangu huu katika sehemu zingine nchini, na hata ningependa kutoa mafunzo kwa madume wenzangu ili pia wao wazidi kunufaika na uhondo pasipo kukumbwa na wasiwasi wa kulipia”.