Makala

FUNGUKA: 'Napenda kunusa chupi za mpenzi…'

August 10th, 2019 2 min read

Na PAULINE ONGAJI

WANAUME wengi watakuambia kwamba mojawapo ya mambo yanayowavutia sana kwa mwanamke ni usafi, na hasa wa mwilini.

Na hakuna kitu kinachoakisi usafi hasa wa mwanamke kama kuvalia chupi safi, suala linaloafikiwa kwa angaa kubadilisha vazi hili mara moja kwa siku.

Lakini sio kwa Ben. Kabla ya kukuhadithia tabia yake, acha kwanza nikutambulishe kwa kaka huyu mwenye umri wa miaka 35.

Mbali na ngozi yake ya lami ambayo ni laini na inayong’aa, mashavu yake yamechomoza kana kwamba Mungu aliyachonga kwa utaratibu na ukamilifu.

Macho yake meupe pe huku mboni nyeusi ti zikichomoza, suala linalomfanya kuonekana hata akiwa mbali.

Tabasamu yake ya kipekee inafichua meno yake meupe yaliyojipanga kama jeshi kwenye gwaride.

Tukisonga chini kidogo, bwana huyu amebarikiwa kwa umbo la kipekee. Kifua kipana huku misuli yake thabiti ikichomoza kila anapovalia shati linalombana.

Kimavazi pia yeye sio mshamba, kwani anafahamu mitindo inayokumbatia vyema umbo hilo lake la kupendeza.

Katika masuala ya usafi, hajaachwa nyuma. Kila mara nywele zake huwa zimenyolewa vilivyo huku ndevu zake zikichanjwa kikamilifu kuambatana na mashavu yake.

Usidhani kwamba kwa sababu kajaliwa kimaumbile, basi akili kanyimwa. La! Ben ni mwerevu. Shuleni alifanya vyema, suala lililomhifadhia nafasi katika mojawapo ya vyuo vikuu maarufu nchini ambapo alisomea masuala ya kifedha na uhasibu.

Na katika harakati hizo, mwanzoni alipata ajira kama mkuu wa idara ya fedha katika kampuni moja ya kimataifa, kabla ya kupanda madaraka ambapo kwa sasa yeye ni afisa mkuu mtendaji.

Kutokana na kazi yake nzuri, pesa sio shida, na hivyo sifa hizi zote zikichanganywa, Ben anakuwa kivutio ajabu kwa mabinti wengi.

Lakini licha ya kutamaniwa na mabinti kibao, ameshindwa kudumisha uhusiano wowote anaoingia ndani, hasa kutokana na kichocheo chake cha ajabu cha mahaba.

“Sipendi mabinti wanaodumisha usafi wa kisima cha uzima, na hasa inapowadia wakati wa kusafisha chupi. Navutiwa na mavazi haya yakiwa bado na uchafu.

Nafurahishwa na harufu halisi inayotoka kwenye sehemu hii. Kutokana na sababu hii, sitaki hata siku moja usafishe chupi yako baada ya kuivalia.

Ukiwa mpenzi wangu, basi lazima ufuate sharti hili kikamilifu. Kila unapovua vazi hili, unabadilisha na kuvalia lingine pasipo kulifua, ambapo unatarajiwa kulirudia lile chafu baadaye.

Pengine harufu ikikuzidi kiasi cha kushindwa kulivalia, basi nalihamisha kwenye kijisanduku changu chumbani kwa raha zangu.

Japo harufu hiyo ni kero kwa wengine, kwangu ni kivutio kikuu na kichocheo cha mahaba. Ukinifanyia hivyo, itisha chochote katika uhusiano wetu na utakipata.

Lakini licha ya uzuri wangu na mfuko mzito, imekuwa vigumu kwangu kudumisha uhusiano ambapo japo ni wengi wanaovutiwa nami kwa mara ya kwanza, pindi wanapoingia katika uhusiano na kusikia masharti yangu, wanahepa”.