Makala

FUNGUKA: 'Nikiona rinda mwili hutetema'

June 22nd, 2019 2 min read

Na PAULINE ONGAJI

KUNA baadhi ya watu ambao watakuambia kwamba ni nadra kwa wanaume wengi kudumisha uaminifu katika uhusiano mmoja, yaani wanaume waliumbwa kuonja huku na kule.

Edward, 34, anawakilisha asilimia hiyo kwani huenda amevunja rekodi ya mabinti tofauti anaowatafuna, licha ya kuwa ana mke na watoto.

Ameoa na ana watoto watatu, lakini hili halijamzuia kusaka mahaba kwingineko, huku tabia yake ya ukware ikifafahamika sio tu mtaani anakoishi, bali pia kazini.

“Tatizo langu ni kuwa nina ashiki zisizo za kawaida kiasi kuwa sibagui, awe kahaba, mjakazi au mke wa jirani, mfanyakazi mwenzangu au hata rafiki ya mke wangu, mradi tu amevalia rinda.

Siwezi hesabu idadi ya wanawake ambao nimewatafuna. Mtaani ninakoishi nimewatafuna wake za watu, wajakazi, mabinti, wahudumu wa baa, akina mama-mboga na mama-fua, marafiki za mke wangu mara kadha wa kadha.

Sio tu ninakoishi pekee, kwani pia hata kwenye baa ninamoburudika kila wikendi au hoteli, najivunia kuwaonja wahudumu pale.

Napenda kuchanganya mabinti wa kutoka kila haiba ya maisha kwani nahisi ni kana kwamba naonja vyakula tofauti.

Ndiposa utapata kwamba, chaguo langu la mabinti ni pana. Naonja wanaofanya kazi za afisi, wanaouza madukani, wafanyabiashara, wanaouza mboga na hata wajakazi ili kupata vitu tofauti.

Kazini, awe bosi, mlinzi au wafanyakazi wenzangu, mradi nawatamani hakuna ambaye huwa na ujasiri wa kunikwepa hasa ikizingatiwa kwamba nimeumbwa nikaumbika. Mimi ni mtanashati, nina umbo la kipekee na pia kimapato siko vibaya.

Lakini hata mimi nina vigezo ninavyoangalia kabla ya kumchagua binti. Kwanza, lazima awe tayari kukubali kwamba raha zetu hazitaishia katika mwunganisho wowote. Aidha, sharti aelewe kwamba baada ya hapa, hata tukikutana njiani hapaswi kunisalimia wala kuonyesha kwamba ananifahamu.

Tunapokutana pengine mkahawani, baada ya mazungumzo nitapendekeza pahali pa kwenda ili kumaliza haja yetu ambapo tutaelewana kwamba baada ya shughuli, hakuna muunganisho wowote.

Nimetenga Jumatano, Ijumaa na Jumamosi kwa shughuli hii ambapo hupanga mabinti hawa kwenye ratiba kali baada ya kazi.

Ili kushibisha kiu yangu niko tayari kutumia pesa zote mradi nipate ladha tofauti za mabinti, ndiposa katika mshahara wangu nimeweka bajeti ya shughuli hizi.

Na sio kwamba mimi hufanya mambo haya nikiwa nimejificha sana kwani hata mke wangu anajua, na amekubali kwamba hakuna tishio mradi mwishowe nitarudi kwake.

Sipangi kuacha tabia hii na naamini ndio imeniwezesha kudumisha uhusiano mzuri na mke wangu. Nasema hivi kwa sababu simsumbui kila mara anihudumie, hasa ikizingatiwa kwamba amejifungua majuzi tu!”