Makala

FUNGUKA: 'Sipendi warembo wa nywele ndefu'

April 6th, 2019 2 min read

Na PAULINE ONGAJI

WANAUME wengi watakubaliana kwamba nywele ndefu huongeza urembo wa mwanamke.

Ni dhana iliyopo katika baadhi ya jamii na hata dini.

Huenda ni kutokana na sababu hii ndipo utapata kwamba sekta ya nywele ni ya thamani ya mabilioni ya pesa, kwani wanawake wengi wako tayari kufanya chochote kuafikia urembo huu unaohusishwa na nywele ndefu.

Ikiwa wewe ni mmoja wa hao mabinti basi huenda huna nafasi katika maisha ya Stanislaus, dume fulani lililokita kambi eneo la Mombasa.

Kwa Stanislaus hakuna binti anayeudhi kama yule aliye na nywele ndefu.

Lakini kabla ya kukusimulia zaidi hebu kwanza nikutambulishe kwa kaka huyu. Bwana huyu anafanya kazi na mojawapo ya kampuni zinazohusiana na utalii ambapo anahudumu kama meneja.

Mbali na taaluma yake ya kutamaniwa hasa kuambatana na kipato kikubwa inachomvunia, kaka huyu ameumbwa akaumbika ambapo anaakisi sifa zote ambazo humezewa mate na mabinti wengi.

Kifua chake ni kipana huku misuli ikichomoza kote.

Tumbo lake ni bapa, uso wake wa kupendeza, taya zilizobainika usoni, ngozi ya chokoleti, na mashavu ambayo kidogo yanakwaruza, kuashiria kuwa yeye ni dume ambalo bila shaka limekuwa likinyoa ndevu kwa miaka.

Sio hayo tu, Stanislaus, ni mojawapo ya madume wachache wasio na tabia ya kuchovya huku na kule hasa akiwa katika uhusiano.

Lakini usipumbazwe na sifa hizi. Kaka huyu amefanya iwe ngumu kwa mabinti kudumu naye katika uhusiano, kutokana na masharti yake hasa kuhusiana na nywele.

“Sipendi kamwe mabinti wa nywele ndefu. Ikiwa unataka kuwa wangu basi jiandae kunyoa nywele na kichwa chako kisalie kama uwanja.

Napenda mabinti walioonyoa vichwa kwani nataka wakati wa mahaba niweze kugusa kichwa chote pasi na vidole vyangu kusalia na mafuta, vumbi, au harufu inayotokana na jasho kwenye nywele ndefu.

Nataka mwanamke akioga aanze utosini hadi miguuni na kamwe siwezi kuvumilia harufu inayotoka kutoka baadhi ya vichwa vya mabinti hasa wanaopenda kusonga hizo nywele za kubandika. Upara unaashiria usafi kwani hakuna hatari ya chawa au wadudu wengine kupata hifadhi kwenye nywele.

Mbali na hayo, upara ni mbinu mwafaka ya kupunguza gharama. Siku hizi naskia kuna mabinti wanaotumia maelfu ya pesa kwa nywele za kubandika. Kwangu, pesa nyingi ambazo naweza kutumia kwa kicwa cha mwanamke ni Sh50. Play online pokies for free! Whether you’re a seasoned gambler or a newcomer, you are likely to find nonstop entertainment and endless opportunities to win with fun-filled promotions and lots of games in an online casino. To get access to the casino games you have to load your casino account and find where you can login to kings chance casino . You can find a good number of $5 deposit casinos in Australia.

Lakini haimaanishi kwamba ukiwa na nywele ndefu hauna fursa ya kuwa katika uhusiano nami. Fursa ipo, lakini uwe tayari kunyoa hizo nywele pindi tunapokubaliana rasmi kuwa katika uhusiano.”

Cha kushangaza ni kwamba kwa upande wake ameotesha shungi kichwani na anaamini kwamba yeye ni safi sana, na hivyo ana uwezo wa kudumisha usafi wa nywele, akilinganishwa na mabinti ambao anasema hawawezi kuaminika inapowadia katika masuala ya usafi wa kichwani.