Makala

FUNGUKA: ‘Sipotezi muda kutekenya bikira’

May 19th, 2019 2 min read

NA PAULINE ONGAJI

Jamii nyingi ambazo bado zinatawaliwa na itikadi za kale bado zinasisitiza umuhimu wa madume wao kuoa binti akiwa bikira.

Lakini kwa wanaume ambao wamekengeuka na kufunguka kimawazo, ubikira kamwe haufafanui utamu wa tunda wala uzuri wa mwanamke.

Edward ni mmoja wao. Mwanzoni acha nikutambulishe kwa kaka huyu mwenye miaka 34. Edward anafanya kazi ya mauzo katika kampuni moja ya mawasiliano hapa jijini Nairobi ambapo mshahara wake sio mbaya.

Ni suala ambalo limemfanya kuwekeza katika ujenzi ambapo amejenga jumba lake na zingine sita za kukodisha katika mtaa mmoja kwenye barabara kuu ya Thika.

Ukimtazama kwa mara ya kwanza utadhani kwamba ni kaka wa kawaida kwani ni mmoja wa wale madume waonyeshao heshima wakiwa katika maeneo ya umma. Yaani si wale madume wanaowakosea heshima mabinti hadharani, wala kutukanana hasa baada ya kulewa.

Ana mke na watoto watatu. Lakini licha ya kuwa na familia, bwana huyu ni mkware ajabu ambapo hakuna rinda linalompita. Iwe kazini anakofanya kazi, njiani anakopita na hata kwenye mitandao ya kijamii, kaka huyu hachoki kuwinda mabinti, kuwaomba namba zao za simu, na kwa wale wanaoingia kwenye ndoano yake, huwapeleka kwenye lojing’i duni mitaani kuwashughulikia.

“Mimi nimeumbwa nikaaumbika; yaani Maulana kanibariki kwa sura nzuri na umbo la kupendeza, kisha ukiongeza na mfuko wangu mzito, naweza kumpata binti yeyote nimtakaye,” yeye hujigamba kila wakati.

Lakini hili sio jambo linalostaajabisha kumhusu. Kinachoshangaza hata zaidi ni kwamba anapowawinda mabinti, kaka huyu husisistiza kwamba hamtaki bikira.

“Kama watu wajuavyo nimeoa, kumaanisha kwamba haja yangu ni kuramba na kusonga. Kutokana na hilo sitaki bikira anayekuja akiwa na kufuli na kutarajia niwe wa kwanza kufungua lango. Sina haja na binti atakayenipotezea wakati huku akitarajia nimfunze kila jambo.

Simtaki bibi ambaye ataanza kuniambia eti nifunge macho kwanza au tuzime taa. Nataka binti ambaye tukiingia chumbani hatoona aibu. Napenda mwanamke anayekuja na ushupavu na mbinu za kila aina bila woga. Sio yule atanipotezea muda na kunisumbua eti kwa sababu hajazoea.

Wikendi inapokaribia, mimi huwa na shughuli nyingi za kusaka mabinti kadha na hivyo sina wakati wa kupotezewa na binti msumbufu.

Mara kwa mara nimekumbana na mabikira lakini pindi ninapogundua hivyo, mimi huwasepa na kuwaambia kwanza wapate ustadi na uzoefu kabla ya kunitafuta. Hata hivyo hakuna binti ambaye nimewahi kumfukuza kisha akarejea.

Naamini kwamba ubikira ni jambo ambalo kamwe haliwezi dumishwa daima dawamu, na ikiwa ni hilo unalofuata kutoka kwa mwanamke, basi utajinyima mengi maishani”.