Makala

FUNGUKA: Starehe yangu vijana barobaro

April 12th, 2019 2 min read

Na PAULINE ONGAJI

UNAPOMTAZAMA Venice utadhani kuwa ni mwanamke wa kawaida na mwenye heshima zake.

Bibi huyu ana umri wa miaka 33 na anamiliki biashara ya saluni kubwa jijini Nairobi.

Katika saluni hiyo pia ameanzisha chuo kidogo cha kutoa mafunzo ya ususi na urembo.

Ameolewa na ana watoto watatu huku mumewe ambaye ni mfanyabiashara mkubwa akihakikisha kwamba mahitaji ya mkewe na wanawe yanakidhiwa vilivyo.

Amemnunulia gari kubwa ambalo kila wiki analijaza mafuta. Pia, anagharamia mavazi yake na watoto wao, mbali na kununua chakula na kulipa karo, kumaanisha kwamba pesa anazounda bibi huyu ni zake tu.

Kila baada ya miezi mitatu binti huyu hupewa fursa ya kubadilisha mavazi yake na kupata mapya. Kwa upande mwingine anapewa fursa ya kubadilisha gari baada ya miaka mitatu, vyote kwa gharama yake mumewe.

Wengi watadhani kuwa kwa binti anayeshughulikiwa hivi basi hana budi ila kutulia katika ndoa, lakini sio Venice.

Tamaa ya binti huyu kwa madume baru baru imekolea kwenye mishipa yake ya damu.

Mtaani kote anafahamika kwa tabia yake ya kuwagawia vijana asali kabla ya kuwatema.

Mlo wake unahusisha wanafunzi wanaoletwa hapo kazini kujipa ujuzi, madume wapya anaowaajiri hapo kazini, manamba wa matatu, miongoni mwa madume wengine barubaru wasiosita kulambishwa asali.

Kwa hao wanafunzi ahadi anayotumia ni kuwa atawapa kazi lakini mara nyingi nia yake hapa huwa ni burudani tu, na swali kuu ni mbinu zipi anazotumia kuwanasa?

“Kwa upande wa wanafunzi unachohitajika kufanya ni kuwapeleka lanchi mara kadha na kuwadanganya kuwa utahakikisha kuwa wanaajiriwa.

Lakini baada ya kuwapa fursa ya kuchovya mara kadha unawatema bila ilani. Kwa kawaida wanafunzi hawa wako hapa kwa miezi mitatu au minne kwa hivyo muda huu ukikamilika watakutoa wapi?

Ili kunitembelea baadaye, mgeni atahitajika kupata kiingilio ambacho atapewa tu iwapo mimi mwenyewe nitaidhinisha.

Baada ya kunitumbuiza, sina wasiwasi kwani kwa kawaida hakuna ninayemlazimisha, ni ushahidi upi watatoa dhidi yangu?

Nikianzisha uhusiano na kaka hapo kazini, nampa mamlaka na kuhakikisha kwamba anayatumia kuwakera wenziwe. Hii ni silaha mwafaka kwani akikumbwa na tatizo kazini hakuna atakayetaka kumsaidia.

Mbali na pesa ninazowapa, mamlaka haya pia huwafanya wakwepe kufanya kazi kama wanavyohitajika, suala ambalo mara nyingi hufanya baadhi yao hata kukosa kuja kazini kama inavyohitajika.

Wao wanadhani kuwa hayo ni mapenzi kumbe ni ujanja wangu wa kukusanya ushahidi tosha nitakapotaka kuwatimua kwa sababu ya utepetevu.

Kwa upande mwingine nafurahia hawa vijana barubaru kwani wana nguvu wakilinganishwa na mume wangu. Ni suala ambalo kwa kawaida analifahamu kwani anajua kuwa wako hapo tu kwa muda, na moyo wangu ni wake.”