Makala

FUNGUKA: ‘Ukija kwangu nguo ziache mlangoni!’

July 4th, 2020 2 min read

Na PAULINE ONGAJI

KATIKA masuala ya mapenzi, watu wamejulikana kujihusisha na mambo mbalimbali – mengine yasiyochukuliwa kuwa ya kawaida – ili kushibisha kiu yao ya mahaba.

Jackson ni mmoja wao.

Kwa miaka, amekuwa akijihusisha na tendo la kushangaza kama mbinu ya kuchochea ashiki nyumbani kwake.

Jackson, anasisimuliwa na mabinti wanaotembea uchi wa mnyama wakiwa nyumbani kwake.

Jackson ana umri wa miaka 37 na anafanya kazi kama mkurugenzi wa taasisi moja kubwa jijini Nairobi.

Ni kazi aliyopata baada ya kuhitimu chuoni mwongo mmoja na nusu uliopita ambapo alifanya vyema sana alipokuwa anasomea shahada yake.

Akiwa katika shule za msingi na upili, Jackson alikuwa mojawapo ya wanafunzi werevu sana, suala lililomhifadhia nafasi katika chuo kikuu kimoja hapa jijini.

Ustadi wake kimasomo, pia ulimnasia nafasi ya ufadhili wa kimasomo, kusomea shahada ya uzamili katika chuo kikuu kimoja nchini Uingereza.

Lakini kando na masuala ya elimu, Jackson ameumbwa akaumbika, huku utanashati wake ukiwa kivutio cha mabinti wengi wanaopata fursa ya kukutana naye.

Hata hivyo, sawa na tujuavyo kwamba hakuna kizuri kisicho na doa, kaka huyu hajakosa udhaifu. Jackson ana tatizo la kusalia katika mahusiano ya kimapenzi, suala linalotokana na tabia yake isiyo ya kawaida, kama anavyoeleza zaidi:

“Nafurahia mwanamke anayetembea uchi wa mnyama akiwa nyumbani. Ikiwa unataka kuwa mpenzi, mchumba na hatimaye mke wangu, unapaswa kuelewa kwamba mwanamke aliyevalia nguo nyumbani ni kero kwangu.

Hii inamaanisha kwamba, kama mpenzi au mke wangu, unapaswa kukubali kwamba pindi unapowasili nyumbani kutoka shughuli zako, hapo hapo mlangoni unapaswa kuvua nguo zote na kusalia vivyo hivyo.

Shughuli zako za nyumbani, iwe kufua au kupiga deki, zote zifanywe ukiwa uchi. Hasa nafurahia chakula changu kikiandaliwa na mwanamke aliye uchi wa mnyama kwani hii huniongezea hamu ya kula chakula hicho.

Aidha, kutembea uchi wa mnyama kunaniongezea ashiki, na hivyo kuongeza uhondo tunapoanza mahaba.

Suala la mwonekano sio tatizo, uwe na umbo la chupa au la, naelewa kwamba maumbile ni kazi ya Mungu.

Lakini kuna masharti pia ambayo lazima yafuatwe. Kwa mfano, lazima binti udumishe usafi, hivyo, pindi unapoingia nymbani na kuvua nguo, unaelekea bafuni na kuoga kabla ya kuanza shughuli za nyumbani.

Nimethibitisha mara kadhaa kwamba kila mwenzangu anapokosa kuzingatia haya, penzi langu kwake hutoweka.

Ni suala ambalo limeninyima fursa kadhaa za kupata mke kwani kila ninapokutana na binti na kumpa masharti haya, anayafuata kwa muda, lakini baadaye anashindwa na kushika njia.

Hata hivyo, nina matumaini katika harakati za kutafuta mke atakayekumbatia masharti yangu na hatimaye kukubali kuwa mke wangu.”