FUNGUKA: ‘Uungwana achia wazee wa kanisa’

FUNGUKA: ‘Uungwana achia wazee wa kanisa’

Na PAULINE ONGAJI

KRIS 48, ameoa na kutalikiana mara tisa na anakiri kuwa sasa hana haja na wanawali bali tamaa yake ni wake za watu.

Tayari ana watoto 12 lakini asema bado hajampata anayemfaa kwani kwake wanawake hawaaminiki.

Tangu kuvunjika kwa ndoa yake ya mwisho miaka minne iliyopita, ametoka na mabinti 19, wote wake za watu.

Baada ya talaka yake ya tisa na kuwasikia marafiki zake wakilalama kila mara kuhusu kulaghaiwa na wake zao, hapo ndipo alifuta imani kwa wanawake na sasa anasadiki udanganyifu ni maumbile ya kike.

Kris ambaye ni msimamizi mshiriki katika shirika moja la kimataifa ana haya ya kusema.

“Kwangu hakuna mwanamke wa kuaminika kwani wote watakuahidi hili na kufanya lingine.

Ni sababu hii ambayo imeelekeza hamu yangu kwa wanawake walioolewa na hasa waliohalalisha ndoa zao.

Nia yangu sio kuharibu nyumba za watu lakini nawavizia kwa sababu najua wanawake hawaaminiki na hata nikimtafuna mmoja leo, sio wangu na hivyo sitahisi machungu ya kulaghaiwa.

Sina muda wa wanawali ambao watakuja kwangu wakiwa na matumaini ya kutaka raha yetu ya muda kugeuka uhusiano wa kudumu. Nafasi yangu ni kwa wanawake wanaojua kwangu ni ngoma pekee kisha warudi kwa waume zao.

Ninapoanza kumvizia mke wa mtu hakuna kudanganyana kuwa raha zetu zitageuka penzi la muda mrefu kwani mwishowe atarudi kwa mumewe nami nitarejea kwangu bila mzigo wowote moyoni.

Uhusiano wangu na wake za watu hautatanishi mradi anataka uhondo pekee.

Kumbuka kwamba mimi hufurahia ngoma tu lakini ninaposhuku kana kwamba unaanza kuvutiwa nami, nitakusepa mara moja.

Aidha, katika uhusiano wa aina hii, hakuna matumaini ya binti kukufuata umpe hela kwani anajua kwamba ni raha ya muda tu. Lakini katika pilkapilka zangu ni mimi nakumbwa na jukumu la kulipia chumba na kununua vinywaji na hata kumpa binti nauli ya kurejea kwa mumewe.

Hakuna umri hususan ninaolenga, iwe una umri wa miaka 20, 30, au 90, mradi una mume, basi umefuzu kuingia ugani mwangu.

Naamini kuwa wanawake hawakuumbiwa mwanamume mmoja, ndiposa sitaki kuwa huyo anayehangaika kutafutia pesa mwanamke mmoja ila tu kuishia kulaghaiwa na kuchezewa pembeni.

Ni mbinu ambayo nimetumia kwa muda sasa bila tatizo kubwa. Kuna wakati ambapo mambo huwa sio shwari kwani kuna baadhi wanaotafunwa na kudhani kuwa sasa twaweza anza uchumba. Ole wako ukija kwangu na nia kama hiyo.

Iwe mtaani, njiani au kazini, mke wa mtu ni windo tosha.

Hata uwe rafiki yangu, mradi tu umenionyesha mkeo, nakuhakikishia kwamba hatimaye nitamtafuna.

Kuna wanaoniuliza ni vipi nimeweza kuwashawishi wanawake hata wenye misimamo mikali na ndoa thabiti kuingia boksi? Jibu ni nyama ya ulimi, mwonekano wa kipekee, vile vile mechi za kusisimua”.

You can share this post!

Kabras na KCB watinga fainali ya raga ya Kenya Cup baada ya...

CHOCHEO: Ukitunzwa, jitunze!