Furaha mwanamume aliyetoweka miezi 8 iliyopita akirejea

Furaha mwanamume aliyetoweka miezi 8 iliyopita akirejea

Na WAWERU WAIRIMU

MFANYABIASHARA wa Isiolo aliyetoweka kwa njia ya kutatanisha siku ya Krismasi mwaka 2020, amerejea kwake na kuungana na familia yake.

Bw Abduba Boru Waqo aliwasili nyumbani kwake viungani mwa mji wa Isiolo, Alhamisi asubuhi, miezi minane baada ya kutoweka.

Urejeo wake uliwashtua wakazi na kuwafurahisha jamaa zake ambao walikongama nyumbani kwake haraka.

Bw Boru maarufu kama Abuya aliripotiwa kutoweka alipokuwa akielekea nyumbani mwendo wa saa moja na nusu za usiku mnamo Desemba 25, 2020.

Alikuwa ametoka katika biashara yake ya buchari ambako alishinda mchana kutwa akiwa na wanawe pamoja na kakake.

Mfanyabiashara huyo alikuwa na Sh35,000 wakati huo, pesa ambazo zilitokana na mauzo yake ya nyama siku hiyo.

Aliwatangulia wanawe ambao walisalia nyuma.

Lakini walipofika nyumbani dakika 30 baadaye, hakuwepo na ukawa mwanzo wa kutoweka kwake.

You can share this post!

Wanafunzi wazimia shuleni kwa njaa

Gor Mahia yawasaka wavamizi 3 nje ya nchi