Gachagua aahidi kuimarisha usalama eneo la Kerio Valley

Gachagua aahidi kuimarisha usalama eneo la Kerio Valley

NAIBU Rais Rigathi Gachagua mnamo Jumamosi aliwahakikishia wakazi wa Bonde la Kerio kuwa serikali ya Kenya Kwanza itajizatiti kukabiliana na utovu wa usalama ambao umedumu eneo hilo kwa muda mrefu.

Bw Gachagua alisema kuwa baada ya wiki mbili, Waziri wa Usalama wa Ndani na Katibu katika wizara hiyo watakuwa wameteuliwa na kibarua chao cha kwanza kitakuwa kuhakikisha usalama umerejea katika eneo la Bonde la Kerio.

Akizungumza katika mazishi ya Naibu Gavana wa Baringo Charles Kipng’ok eneobunge la Eldama Ravine, Naibu Rais pia aliahidi kuongoza mkutano wa viongozi kutoka eneo hilo ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa utovu wa usalama.

Kati ya mikakati ya kudumisha usalama kwenye Bonde la Kerio, ni kuwaongeza maafisa wa usalama na pia kushughulikia tatizo la maji ambalo limesababisha uhasama kati ya jamii za wafugaji.

Pia Bw Gachagua aliahidi kuwa serikali yao itaimarisha shughuli za kilimo ndiposa imeshatoa mbolea nafuu.

  • Tags

You can share this post!

Kipchoge aifuta rekodi ya dunia ya kilomita 42 kwa nusu...

Sitakuwa dikteta, Ruto aondoa hofu

T L