Gachagua amtetea Ruto kwa kumteua mgombea mwenza

Gachagua amtetea Ruto kwa kumteua mgombea mwenza

NA KENYA NEWS AGENCY

MBUNGE wa Mathira, Bw Rigathi Gachagua, amemtetea Naibu Rais William Ruto kwa kumteua kama mgombea mwenza wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Dkt Ruto anawania urais kwa tiketi ya chama cha United Democratic Alliance (UDA).

Bw Gachagua, ambaye alifanikiwa kuwashinda watu wengine watano waliokuwa wakiwania nafasi hiyo, alisema hakupendelewa hata kidogo.

Badala yake, alihoji kuwa Dkt Ruto alimteua kutokana na tajriba yake pana katika utumishi wa umma na sifa ya kuchapa kazi kwa bidii.

Alisema hilo ndilo lilimwezesha kuibuka mshindi dhidi ya wenzake.

Akijitetea kama mtu aliyetoka katika familia maskini hadi alipofikia, Bw Gachagua alisema yeye ndiye anayefaa zaidi kupewa nafasi hiyo.

“Ninajua vile serikali inaendeshwa. Nitatumia ujuzi huo kumsaidia Dkt Ruto kuendesha serikali baada yetu kutwaa ushindi kwenye uchaguzi. Nimefanya kazi naye kwa zaidi ya miaka 25, hivyo ninaamini hatutakuwa na tatizo lolote. Nitakuwa naibu rais mzalendo kwake,” akasema mbunge huyo kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha Inooro.

Bw Gachagua pia alipuuzilia mbali madai ya kumsaliti Seneta Kindiki Kithure (Tharaka Nithi), ambaye ndiye alipigiwa upatu zaidi kutwaa nafasi hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Himizo Mkaguzi ashirikishe umma huku akizindua nakala ya...

Ukimwi: Himizo watu waendelee kubaini hali zao

T L