Gachagua apingwa kuhusu kauli ya misitu

Gachagua apingwa kuhusu kauli ya misitu

NA WAANDISHI WETU

NAIBU Rais Rigathi Gachagua leo ataongoza mkutano kupata njia ya kukabiliana na ukame ambao umesababisha njaa nchini na utunzaji wa mazingira.

Mkutano huo unakuja siku mbili baada ya Bw Gachagua kuwaambia Wakenya warejelee kilimo misituni.

Mnamo Jumamosi akiwa katika Kaunti ya Baringo, Naibu Rais alisema kuwa Wakenya wanastahili waruhusiwe kuendeleza kilimo msituni ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

Kwa kulima msituni na wakati huo huo kuutunza, Bw Gachagua alidai gharama ya maisha itapungua kwa sababu Kenya itajitoleza kwa chakula.

Rais William Ruto ndiye aliamuru mkutano wa leo Jumanne uandaliwe.

Inakadiriwa watoto 942,000 na akina mama 134,000 wanaonyonyesha wanakabiliwa na utapiamlo kwa sababu ya ukosefu wa chakula cha kutosha.

“Naibu wangu Rigathi ataongoza mkutano na maafisa wa serikali na viongozi ili kutafuta njia ya kupambana na athari za ukame. Pia watakumbatia mapendekezo ya kuwaokoa wakazi wanaokabiliwa na njaa kwenye kaunti 20,” akasema Rais Ruto kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo, kauli ya Bw Gachagua imezua cheche huku seneta wa Narok Ledama Ole Kina akisema atapinga juhudi za raia kuruhusiwa kulima ndani ya msitu wa Mau.

Wanasiasa wengine pamoja na wataalamu pia wamepinga mpango aliotangaza Bw Gachagua wakisema utachangia katika uharibifu wa misitu.

Walieleza kuwa mpango huo ulitukika miaka ya awali kunyakua mashamba katika misitu ya serikali.

  • Tags

You can share this post!

Mkenya Karan Patel aibuka mshindi wa Rwanda Mountain...

TUSIJE TUKASAHAU: Sakaja atueleze jinsi anavyopanga...

T L