Gaidi mtoro asema atahepa Kamiti tena akipata mwanya

Gaidi mtoro asema atahepa Kamiti tena akipata mwanya

Na SIMON CIURI

MMOJA wa magaidi watatu waliotoroka gereza kuu la kamiti Novemba 15 aliambia mahakama ya kesi za ugaidi kwamba, akipata fursa, atahepa tena kwa vile anahofia atauawa na maafisa wa polisi wa kupambana na ugaidi akikamilisha kifungo.

Musharraf Abdalla Akhulunga, almaarufu Zarkarawi aliyekuwa ametoroka akiwa na Mohammed Ali Abikar na Joseph Juma Odhiambo almaaruf Yusuf, aliungama mbele ya Hakimu Mkuu Bi Diane Mochache kwamba, iliwachukua mwaka mmoja unusu kupanga jinsi ya kutoroka.

Wote watatu wanatumikia kifungo cha jumla ya miaka 78 kwa kushiriki katika visa vya ugaidi.

Abikar alikuwa mmoja wa magaidi walioshambulia Chuo Kikuu cha Garissa ambapo wanafunzi 148 walipoteza maisha yao.

“Nikipata nafasi nitatoroka. Tulikamatwa kwa vile nguvu zilikuwa zimetuishia. Tulikuwa dhaifu na hatukuwa na chakula. Tulikuwa tunaelekea Ethiopia. Tulikuwa tunasaka uhuru na usalama kwa vile hakuna haja ya kukamilisha vifungo kisha polisi wanatukabidhi mikononi mwa polisi wa kupambana na ugaidi watuue,” Musharaf alieleza mahakama.

Aliongeza kusema, “Hata magaidi ambao wamerekebika na kukamilisha vifungo waliuawa. Tulikuwa tunatafuta usalama.”

You can share this post!

WANYONYI CUP: Red Carpet, Uthiru, WYSA zasonga mbele...

Wawaniaji wapigania Kalonzo Ukambani

T L