Michezo

Garnacho, demu wake hawapikiki tena chungu kimoja

January 27th, 2024 2 min read

NA CHRIS ADUNGO

KIPUSA Eva Garcia amezua tetesi za kutengana na kiungo wa Manchester United, Alejandro Garnacho, kupitia ujumbe wake wa hivi majuzi kwenye mtandao wa Instagram.

Mrembo huyo alichapisha ‘selfie’ na mtoto wao akaandika: “Sasa ni wewe na mimi pekee tumeachwa tuchuane na ulimwengu huu katili.”

Ni ujumbe uliochochea wafuasi wa Eva, 18, na Garnacho, 19, kutaka kujua kulikoni na wakabaini demu aliacha kumfuata sogora huyo wa Argentina kwenye mitandao.

Ufichuzi huo ulisukuma baadhi ya wafuasi kudadisi zaidi huku mmoja akiuliza: “Je, ni nini kilifanyika? Na mbona ukaruhusu?”
Mwingine aliongeza: “Garnacho, ni nini umefanya hadi yakafikia hapo?”

Tangu Eva apakie mtandaoni ujumbe wa kudokeza ametemana na dume lake, Garnacho hajasema lolote huku ikifichuka kuwa chapisho lake la mwisho kwenye Instagram ni la kumtakia mamake bathidei murua wiki tatu zilizopita.

Garnacho na Eva walisherehekea kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza mnamo Oktoba 2023.

Hata hivyo, shabiki mmoja wa kike alipania kutumia fursa ya uvumi huo wa Garnacho na Eva kutengana ili kupata mwanya wa kuanza “kumuondolea mwanasoka huyo kijibaridi cha upweke.”

“Najitolea kabisa kuja kwako nyumbani nianze kukupikia chakula ukipendacho. Ule vya mezani na vya chumbani shibe yako! Kwa kuwa mmetengana, Garnacho naomba ulizingatie hili ombi langu kwa dharura.”

Tangu Eva apakie mtandaoni ujumbe wa kudokeza kuwa ametemana na dume lake, Garnacho, 19, hajasema lolote huku ikifichuka kuwa chapisho lake la mwisho kwenye Instagram ni la kumtakia mamake maadhimisho murua ya bathidei wiki tatu zilizopita.

Garnacho na Eva, ambaye anajivunia zaidi ya wafuasi 534,000 kwenye Instagram, walisherehekea kuzaliwa kwa mtoto wao wa kwanza mnamo Oktoba 2023.

Sogora huyo alipakia mtandaoni picha za kupendeza zikimuonyesha akikumbatia mtoto Enzo akiwa kwenye kitanda cha hospitalini. Idadi kubwa ya wanasoka wenzake kambini mwa Man-United walimtumia pongezi na jumbe za heri kwa kujaliwa kimalaika.

Ingawa Garnacho na Eva waliweka bayana uhusiano wao wa kimapenzi mnamo 2021, inakisiwa kuwa walianza kula bata mapema zaidi. Walitangaza kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza mnamo Aprili mwaka jana kisha wakaandaa karamu ya kufichua jinsia ya mtoto siku chache baadaye.

Mkesha wa Mwaka Mpya wa 2024, Garnacho alichapisha kwenye Instagram picha yake akiwa amebeba Enzo kifuani na kuandika: “2023 ulikuwa mwaka wa furaha sana. Ni mwaka ambao sitasahau kwa kuwa maisha yalinipa kitu kizuri na cha maana. Sijui mbele kulivyo ila naona wingu jeusi linalobeba giza katika safari ya mapenzi.”