GASPO Women ya KWPL yasajili 10

GASPO Women ya KWPL yasajili 10

NA RUTH AREGE

KLABU ya Gaspo Women ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL), imesajili wachezaji 10 tayari kwa maandalizi ya msimu wa 2022/23 wa ligi ya wanawake ambao haijulikani utaanza lini.

Lydia Akoth almaarufu ‘Ozil’ na Valentine Khwaka wamejiunga na klabu hiyo wakitokea Zetech Sparks.

Diana Cheptoo, Phanice Kwamboka, Jane Awino, Jackline Nambagara, Josephine Imungu, Noera Milimu na Nuru Adimah wametokea Nakuru City Queens. Ann Arusi pia amesajiliwa na klabu hiyo kama mcheza huru.

Wakati huo huo, wachezaji watatu wameondoka rasmi kwenye klabu hiyo. Kiungo Corazone Aquino alijiunga na Simba Queens ya Tanzania, Hellen Awino alihamia ligi ya kaunti nae kipa Pauline Kathuruh alijiunga na Yanga Princess ya Tanzania.

Meneja mkuu wa klabu hiyo Edward Githua amedhibitisha sajili za wachezaji hao.

“Nimefanya sajili ambazo nina imani zitaleta matokeo mazuri msimu ujao. Sajili hizo nimefanya kwa umakini mno ili ya msimu jana yasitukute tena. Tulishindwa kutwaa ubingwa kwa sababu tulianza msimu vibaya. Tumerekebisha makosa na kwa sasa tupo tayari kupambana,” aliongezea Githua.

“Wakati huu hatuna uhakika ligi itaanza lini, huku kunafanya tushindwe kujipanga mapema. Viongozi wa kamati ya mpito wamekataa kupokea simu zetu wala kujibu jumbe zetu. Hatuelewi kinachoendelea , hakuna dalili zozote za kuanza ligi wiki ijayo. Sisi tutaendelea tu kufanya mazoezi,” alisema Githua.

Aliyekuwa kocha wa timu hiyo Dommie Tilah, alijiuzulu mwishoni mwa msimu jana baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi. Githua anasema klabu hiyo iko mbioni kusaka kocha mwingine.

  • Tags

You can share this post!

Jentrix Shikangwa na beki Ruth Ingotsi watarajiwa kujiunga...

Richarlson aongoza Brazil kupepeta Ghana katika mechi ya...

T L