Gavana apongeza hatua za kufufua sekta ya korosho

Gavana apongeza hatua za kufufua sekta ya korosho

NA KNA

GAVANA wa Kwale, Bw Salim Mvurya, amesifu hatua zilizopigwa katika juhudi za kufufua kilimo cha mikorosho, baada ya soko jipya kupatikana Slovakia.

Akizungumza alipokutana na Balozi wa Slovakia nchini, Katarina Leligdonova, gavana alisema watazidi kushirikiana na wadau wengine kustawisha kilimo.

Mradi wa kuzalisha korosho unaendelezwa mjini Mwangwei, huku kasha la kwanza likitarajiwa kupelekwa Slovakia karibuni. kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali ikiwemo la Ten Senses.

Bw Mvurya alisema kasha la kwanza la korosho linatarajiwa kusafirishwa hadi Slovakia hivi karibuni.

You can share this post!

Pombe ya mnazi yaleta dhuluma kwa wasichana

Jamii yalalamika kutatizwa na operesheni ya usalama Boni

T L