Gavana Lenku aitaka serikali kuu kutoa msaada wa chakula

Gavana Lenku aitaka serikali kuu kutoa msaada wa chakula

NA KENYA NEWS AGENCY

GAVANA wa Kajiado Joseph ole Lenku ameitaka Serikali ya Kitaifa kutoa msaada wa chakula na maji kwa wakazi wa kaunti hiyo ambayo imeathiriwa pakubwa na ukame unaoendelea nchini.

Bw Lenku alisema kuwa maelfu ya wakazi katika kaunti hiyo wanahangaishwa na baa la njaa kutokana na uhaba wa chakula.

Alisema kuwa ukosefu wa malisho na maji umesababisha wafugaji kupoteza mifugo wao.

“Ni maeneo machache sana yaliyopata mvua. Maeneo mengi yangali yanaandamwa na ukame na Serikali ya Kitaifa inafaa kuingilia kati ili kusaidia waathiriwa wa njaa,” akasema Bw Lenku.

  • Tags

You can share this post!

Raila kukita kambi katika ngome ya Mudavadi

MUME KIGONGO: Wataalamu sasa wahusisha ugumba na kansa ya...

T L