Gavana Mwadime alenga utalii kuinua uchumi wa Kaunti

Gavana Mwadime alenga utalii kuinua uchumi wa Kaunti

NA WINNIE ATIENO

GAVANA wa Taita Taveta, Bw Andrew Mwadime, amesema serikali yake inanuia kuwekeza katika utalii ili kufufua uchumi wa kaunti hiyo.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa utalii kuhusu mbinu za kufufua sekta hiyo, Bw Mwadime alisema utalii umedorora katika Kaunti ya Taita Taveta licha ya kuwepo kwa rasilimali nyingi za kuvutia watalii wa humu nchini na wa kigeni zikiwemo mbunga za kitaifa za wanyamapori.

“Tulikutana na wawekezaji wa utalii na biashara kujadili namna ya kufufua utalii. Taita Taveta imepoteza hadhi yake ya kuwa kitovu cha utalii kwa sababu hatujavalia njuga utalii kikamilifu,” alisema Bw Mwadime.

Alisema kaunti yake inaweza kuvuna mapato zaidi kutokana na sekta ya utalii ikiwa itapewa kipaumbele.

“Taita Taveta ni kati ya kaunti tajiri zaidi nchini Kenya na ni lazima tusake namna ya kufufua utalii,” alisema.

Mwekezaji wa utalii, Bw Willy Mwadilo, aliahidi kushirikiana na wawekezaji wengine wa sekta hiyo ili kukuza utalii katika kaunti.

  • Tags

You can share this post!

Afrika huagiza kiwango kikuu cha fatalaiza, matumizi yakiwa...

Wakuzaji minazi nao walilia fidia

T L